Kwa mujibu wa chanzo cha ndani ya jeshi
hilo, pia Rais Kikwete atatumia nafasi hiyo kuliaga jeshi hilo kwa vile
Oktoba, mwaka huu, nchi itamchagua rais atakayepokea kijiti chake cha
urais kwa awamu ya tano.
Msingi wa habari hii ni wafungwa
wanaotumikia kifungo cha maisha jela kwa makosa ya ulawiti na ubakaji,
wanamuziki Nguza Vicking ‘Babu Seya’ na mwanaye, Johnson Nguza ‘Papii
Kocha’ kwani katika hafla kama hiyo, mwaka jana, walimtumia salamu JK
wakimwomba awasamehe kwani walishatambua makosa yao.
“Je, rais hawezi kuitumia nafasi hiyo kuwaachia huru wanamuziki, Nguza
Vicking na mwanaye, ‘Papii Kocha’ ambao wanatumikia kifungo cha maisha
jela?
”Chanzo: “Mh! Sina hakika sana. Maana kama hilo lipo ina
maana ni jukumu la rais mwenyewe na mipango yake kwa mujibu wa katiba,
rais ana mamlaka ya kumsamehe mfungwa kwa kosa lolote lile.”
No comments:
Post a Comment