Kadhalika,
Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, ametajwa kuwa ndiye kiongozi
wa siasa aliyeshuhudiwa na wananchi wengi katika hotuba zake kuliko
wanasiasa wengine waliokwisha kutangaza nia.
Hayo
yamo katika ripoti ya utafiti uliofanywa na Shirika la Maendeleo la
Utafiti la Elimu (Tedro), iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam jana.
Akizungumza
katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Jacob Katerri, alisema
ripoti hiyo ilijumuisha Wilaya 20 na kuwahoji watu 2,000 kutoka
vijijini na mijini.
Alisema
katika ripoti hiyo kipengele cha watangaza nia walioshuhudiwa na watu
wengi katika hotuba, Lowassa anaongoza kwa kushuhudiwa kwa asilimia 54,
akifuatiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Bernard Membe (46), Naibu Waziri wa Fedha , Mwigulu Nchemba (44),
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira (40) na Jaji Mkuu
mstaafu Augustino Ramadhani(39).
Naibu
Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba(34), Waziri Nchi Ofisi
ya Rais, Profesa Mark Mwandosya (31), Mbunge wa Bunge la Afrika
Mashariki, Makongoro Nyerere (27), Waziri wa Ujenzi, John Magufuli
(23), na Mbunge wa Sengerema, Willium Ngeleja (19) na wengine wakifuata.
Katika
Kipengele cha kupunguza tatizo la ajira, ripoti hiyo ilieleza kuwa
wananchi walipohojiwa walieleza kuwa wana imani na Lowassa kwa asilimia
19, Nchemba (14), Magufuli (13).
Makamba
(13), Membe (12), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (10), Mwandosya (7), Dk.
Harrison Mwakyembe (7), Wassira (2) na wengine (3).
“Utafiti
huu umebaini kuwa watangaza nia wengi pamoja na mambo mengine
walijikita sana katika kusema watatatua tatizo la ajira kwa vijana,”
alisema Kaserri.
Kadhalika
ripoti hiyo ilizungumzia kipengele cha kuinua elimu nchini, ambacho
wananchi waliohojiwa walitoa nafasi kubwa ya uwezekano wa kutekelezewa
kwa kipaumbele hiki kwa Lowassa kwa asilimia 25.
Nchemba (18), Membe (16), Makamba (13), Magufuli (12), Mizengo Pinda (12), Wasira (3) na wengine (9).
Pia
ripoti hiyo ilizungumzia kipengele cha Tanzania kuwa nchi ya kipato cha
kati ifikapo waka 2025, na wananchi walikuwa na imani na Nchemba kwa
asilimia 13.4 kuwa ataweza kulipeleka taifa kufikia kipato cha kati.
Lowassa
(11), Wasira (9), Membe (9.20), Magufuli (9.0), Makamba (5.3),
Mwandosya (4.60), Pinda (3.5) na Dk. Mwakyembe (1.40).
Hata
hivyo, utafiti huo ulielezea kipengele cha kuinua sekta ya Kilimo na
Mifugo nchini ambacho kwa watangaza nia hao, wananchi walikuwa na imani
kwa Pinda kwa asilimia 23.
Lowassa
(17), Nchemba (16), Membe (11) Wasira (9), Makamba (7), Magufuli (5),
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (3.3), Mbunge wa Nzega,
Hamisi Kigwangala(3.2) na Mwakyembe (2.6).
Katerri
alisema utafiti huo pia ulihusu kipengele cha Utawala bora na vita
dhidi ya ufisadi ambapo ulionyesha kuwa Mwigulu Nchemba amepata asilimia
17.4 ya uwezo wa kupambana na tatizo hilo.
Wengine waliomfuata ni Magufuli (14.2), Membe (11), Lowassa (6.10), Jaji Ramadhani (6) na Mwandosya (5).
Wengine ni Mizengo Pinda (8), Mwakyembe (8), Makamba (7), Samuel Sitta (6), Dk. Kigwangala (3).
Katika
kipengele za Uadilifu usiotiliwa shaka katika utumishi Nchemba alipata
asilimia 15, Membe (13), Mwandosya (13), Pinda (8), Makamba (8) Jaji
Ramadhani (7), Lowassa (10%).
Katika
kipengele cha hotuba iliyo bora, Katerri alisema Nchemba alipata alama
(A), Wasira( B+), Membe (B+), Mwandosya (B+) Lowassa (B) na Membe (B).
Katerri Alisema lengo la utafiti huo ni kutathmini Elimu katika Nyanja
ya uraia kwa watanzania kupitia vipaumbele katika hotuba za waliokwisha
kutangaza nia kupitia CCM.
Alizitaja
wilaya ambako utafiti huo ulifanyika kuwa ni Kinondoni, Kibaha
Vijijini, Kilombero, Rombo, Arumeru, Mbulu na Babati, Lindi, Mtwara,
Njombe mjini, Njombe Vijijini, Mbeya Mjini, Nyamagana, Biharamulo,
Tabora, Nzega, Bahi, Chamwino na Kasulu.
No comments:
Post a Comment