Inatajwa kuwa kikao kilichofanyika june 23 mwaka huu kati ya
madereva, serikali na wamiliki wa mabasi ndicho kilichozika mgogoro wa
muda mrefu wa kimaslahi ambao ulisababisha uwepo wa migoma ya mara kwa
mara.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa katika kikao cha madereva zaidi
ya 4000 msemaji wa umoja huo Bw Rashid Saleh anasema hatimaye dereva wa
kitanzania amesaminiwa kwa kupatiwa mkataba ambao utamfanya afurahiye
kazi yake.
Aidha katika mkutano huo pia ambao ulitumika kutangaza uanzishwaji
wa chama cha wafanyakazi madereva nchini, madereva walitakiwa
kuhakikisha wanakuwa mstali wa mbele katika kuhakikisha maslahi yao
yanatekelezeka.
Kwa mujibu wa madereva waliozungumza na ITV licha ya kuahidi
kufanya kazi hiyo kwa ustadi mkubwa wamesema kuwa rasimu hiyo ya mkataba
itawawezesha kukidhi mahitaji yao muhimu ambayo wanadai kuyakosa kwa
kipindi cha miaka 50 ya uhuru sasa.
No comments:
Post a Comment