WAZIRI LUKUVI AFANYA ZIARA MKOANI IRINGA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William
Vangimembe Lukuvi ameanza ziara ya siku tatu Mkoani Iringa ambapo
aliongea na watendaji wa Mkoa wa Iringa kuhusiana na migogoro ya ardhi
inayoukumba Mkoa huo . Aidha, Waziri Lukuvi alipata fursa ya kukagua
shughuli za Shirika la Nyumba la Taifa na kusikiliza migogoro ya ardhi
inayowakabili wananchi wa Manispaa ya Iringa na wilaya za jirani za
Kilolo na Mufindi. Katika ziara hiyo, Waziri Lukuvi amerejea kauli yake
aliyoitoa katika mikoa aliyokwishafanya ziara kwa kuwaonya na kuwaagiza
Maafisa ardhi, wapima, wathamini na maafisa mipango miji kuacha mara
moja kujinufaisha kwa kuwadhulumu wananchi haki zao za ardhi. Aidha
ameutaka Uongozi wa Mkoa wa Iringa kuharakisha upimaji wa ardhi ya
wananchi na utoaji wa hati na kutenga muda wao ili kuweza kusikiliza
kero za wananchi ili kupunguza migogoro ya ardhi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment