Rais Dk. Jakaya Kikwete akipokea heshima ya Wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Chuo cha Maofisa Magereza kilichopo Ukonga jijini Dar. |
Rais JK akimpandisha cheo mwanafunzi bora katika kozi ya 21 kutoka Inspekta na kuwa ASP. |
JK aliyasema hayo jana katika shereha za Siku ya Magereza nchini ambapo sherehe hizo kitaifa zilifanyika kwenye Viwanja vya Chuo cha Maofisa Magereza kilichopo Ukonga jijini Dar es Salama na rais ndiye alikuwa mgeni rasmi.
Katika sherehe hizo, Rais JK aliwapandisha maofisa 104 ambao walikuwa wakifanya mafunzo kutoka cheo cha Inspekta na kuwa ASP ambapo kati ya hao 82 walikwa wanaume huku 22 wakiwa maofisa wa kike kati ya hayo 10 wakitoka Chuo cha Mafunzo, Zanzibar.
Rais aliahidi kushughulikia changamoto zinazolikabili jeshi hilo la magereza kabla hajaondoka madarakani na kumwagiza Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja kumwandikia barua Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani mahitaji yao yote ili aweze kuyashughulikia kabla ya kuondoka madarakani.
No comments:
Post a Comment