Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini mkataba wa
makubaliano ya kuwa na soko la pamoja kwa Nchi za Wanachama wa Kanda ya
tatu ya Nchi za Afrika Mashariki, Kusini mwa Afrika na za Magharibi.
Dkt.Bilal pamoja na Viongozi wa Nchi husika wamesaini mkataba huo leo
katika Mkutano mkuu wa tatu wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC), Soko la pamoja la Nchi za Kusini mwa Afrika (COMESA) na Jumuiya
ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwenye Ukumbi wa
Kimataifa wa mikutano wa Sharm El Sheikh, nchini Misri.
Picha zote na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na
Waziri wa Afrika Mashariki, Dkt. Harrison Mwakyembe, akimpongeza baada
ya kusaini mkataba huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na baadhi ya
Mawaziri wake katika mkutano mkuu wa tatu wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC), Soko la pamoja la Nchi za Kusini mwa Afrika (COMESA) na
Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika leo Juni
10, 2015 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Sharm El Sheikh,
nchini Misri.
No comments:
Post a Comment