![]() |
aibu wa Wizara Ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zahra AliHamad |
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
imeahidi kuwalipa walimu walioshiki mafunzo ya kazi za amali Nchini
Iran watapatiwa posho lao wanalodai na kuhakikisha wanapata haki yao ya
msingi . Hayo yameelezwa na Naibu wa Wizara Ya Elimu na Mafunzo ya Amali
Zahra Ali Hamad wakati akimjibu Mh Saleh Nassor Juma Jimbo La Wawi
katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi huko Chukwani aliyetaka kujua ni
sababu gani za msingi zinazopelekea watumishi wa Umma kunyimwa posho zao
wakiwa katika safari kikazi.
Amesema serikali kwa kushirikiana
na Mamlaka ya Mafunzo ya Amali itahakikisha kuwa deni hilo linalipwa kwa
awamu pale hali ya kifedha itakaporuhusu katika mwaka ujao wa fedha.
Amesema kutokana na uhaba wa fedha
uliokabiliwa ya Mamlaka ya Mafunzo ya Amali haikuweza kuwalipa fedha
hizo na badala yake kila mwalimu alilipwa dola 120 na kwa walimu 16
walilipwa jumla ya dola za Kimarekani 1920.
Amesema kuwa jumla ya Walimu 20
wakiwemo 16 kutoka vituo vitatu vya Mafunzo ya Amali watatu kutoka
katika taasisi ya Karume ya Sayansi naTeknolojia na mmoja kutoka Skuli
ya Sekondari ya mikunguni walihudhuria Mafunzo ya kazi za Amali Nchini
Iran kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja.
Aidha alifahamisha kuwa
wafanyakazi hao waliondoka Nchini tangu mwanzoni mwa mwaka jana kwenda
nchini Iran kwa ajili ya mafunzo hayo hadi leo wanadai posho lao hilo .
“Napenda nikiri kuwa kufanyiwa
malipo pungufu ilitokana na kutopatikana fedha za kutosha katika vifungu
vya Mamlaka ya Mafunzo ya Amali, lakini ninakubali kuwa hilo ni deni
ambalo Wizara yangu itahakikisha kuwa walimu wanalipwa haki zao hadi
hivi sasa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali ina shindwa kutekeleza kazi zake
vizuri kutokana na ukosefu wa fedha”, alieleza Naibu hiyo.
Amefahamisha kuwa Mafunzo hayo
yaligharamiwa na Mhisani kutoka Serikali ya Kiislamu ya Iran na Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar ilipaswa kuwalipia posho na fedha za mavazi
kwa mujibu wa taratibu za Serkali .
No comments:
Post a Comment