Malinzi alenga Olimpiki 2020


RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema lengo la kuandaa michuano ya watoto chini ya umri wa 13 ni kushiriki fainali za Michezo ya Olimpiki itakayofanyika jijini Tokyo, Japan mwaka 2020.
Akizungumza kabla ya mchezo wa fainali ya michuano hiyo juzi jijini Mwanza, Malinzi alisema vijana wanaocheza michuano hiyo watakuwa na nafasi ya kucheza timu bora ya taifa ya vijana chini ya miaka 17.
Malinzi alisema watapata nafasi ya kushiriki michuano ya mbalimbali ya watoto. “Mwakani tutaandaa michuano ya watoto chini ya miaka 14.
Watatunzwa watakaoteuliwa wenye vipaji na baada ya hapo watakuzwa vizuri ili kuingia kwenye timu hiyo chini ya miaka 17. “Tunaamini timu ikishiriki Olimpiki, itatusaidia kushiriki michuano mingine mikubwa kama tutaendelea nao,” alisema Malinzi aliyeingia madarakani miaka miwili iliyopita.
Ilala ilinyakua ubingwa baada ya kuilaza Alliance ya Mwanza kwa mabao 3-2, wakati katika mechi ya mshindi wa tatu, Kinondoni iliishinda Mara kwa mabao 2-1.
Michuano hiyo haina kombe kwa kuwa lengo ni kusaidia kupata timu. Katika hatua nyingine, timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars ilicheza na Misri jana usiku katika kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2017 ikiwa ni mechi yake ya kwanza ya Kundi G.
Katika mechi ya kwanza ya kundi hilo juzi Nigeria, mabingwa wa Afrika mara tatu waliifunga Chad mabao 2-0 katika mechi iliyofanyika mjini Kaduna

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved