Marekani kutuma mamia ya majeshi Iraq
Utawala wa Rais Barack Obama wa Marekani unafanya mipango ya kuanzisha
kambi mpya ya kijeshi katika jimbo la Anbar nchini Iraq na kuwatuma
wanajeshi wa kutoa mafunzo na ushauri kuliimarisha jeshi la Iraq ambalo
limekuwa likipambana na wanamgambo wenye itikadi kali wa kundi
linalojiita Dola la Kiislamu, IS. Duru zinaarifu kuwa Rais Obama huenda
akauidhinisha mpango huo wa kuongeza shughuli za kijeshi nchini Iraq hii
leo. Wanamgambo wa IS waliuteka mji mkuu wa jimbo la Anbar wa Ramadi
mwezi uliopita na Marekani inapanga kuweka mikakati madhubuti kuukomboa
mji huo. Marekani ina wanajeshi 3,100 nchini Iraq wanaotoa mafunzo na
ushauri hivi sasa. Rais Obama anatarajiwa kuidhinisha mpango huo wa
kutuma majeshi zaidi nchini Iraq mapema iwezekanavyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment