Makumi wauawa Yemen katika mashambulizi ya Saudia
Makumi ya watu wameuawa katika mwendelezo wa mashambulizi ya kichokozi
ya Saudi Arabia na waitifaki wake nchini Yemen. Jana ndege za Saudia
zilitekeleza hujuma tofauti katika maeneo ya mkoa wa Sada na mikoa
mingine ya Yemen ambapo makumi ya raia wasio na hatia waliuawa na
kuharibu miundombinu na kadhalika makazi na taasisi za serikali. Aidha
ndege za utawala wa Aal-Saud zilishambulia kituo cha mafuta katika mji
wa Razeh mkoani Sada na kupelekea watu wengi kuuawa. Kama hiyo haitoshi
ndege hizo ziliushambulia msikiti mmoj katika mji wa Marwan na kuuharibu
kabisa. Mashambulizi na jinai kubwa za utawala wa Saudia kwa lengo la
kuidhoofisha Harakati ya Kiislamu ya Answarullah ya nchi hiyo na
kumrejesha madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo Abd Rabbuh Mansur Hadi
na aliyeamua kujiuzulu madarakani na kukimbilia Riyadh, yalianza hapo
tarehe 26 mwezi Machi mwaka huu na hadi sasa yameshindwa kufikia malengo
yake. Kwa mujibu wa duru za afya nchini Yemen, zaidi ya watu 4,000
wamekwishapoteza maisha yao wengi wao wakiwa ni raia wasio na hatia.
Katika kujibu chokochoko hizo jeshi la Yemen kwa kushirikiana na
wanamapambano wa kujitolea, limeshambulia kwa makombora kambi za kijeshi
za Malhama na Ainul-Harrah za Saudia na kuangamiza askari kadhaa wa
nchi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment