Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe,
(pichani) amesema sheria tatu za makosa ya jinai zilizo mbioni
kupitishwa na serikali, zimelenga kuwanyamazisha wapinzani kwenye
uchaguzi mkuu ujao, ili wasiweze kuanika madudu ya serikali ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM).
Katika
taarifa yake iliyopatikana jana jijini Dar es Salaam, Mbowe alizitaja
sheria hizo ambazo ama zimesainiwa au zinasubiri saini ya rais kuwa ni
pamoja na ile ya Muswada wa Vyombo vya Habari wa Mwaka 2015, Sheria ya
Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 na Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2015.
Alisema
kuna nia moja tu inayoweza ikaeleza ni kwa nini sheria hizi zimepelekwa
mbio mbio, nayo ni kutokana na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika
Oktoba mwaka huu.(P.T)
“Uwingi
wa sheria hizo mpya kwa pamoja kunaweza kunyamazisha ukosoaji wa
kukosekana kwa utawala bora, na kukandamiza kile ambacho kimekuwa ni
utamaduni wa vyombo vya habari wa kuchunguza na kuripoti ufisadi, ndani
ya serikali,” alisema.
Mbowe
alifafanua kwamba, Muswada wa Vyombo vya Habari wa Mwaka 2015, utawazuia
waandishi wote na vyombo vya habari kujiendesha, kuwa na baraza lao la
habari, isipokuwa waandishi wenye leseni tu.
Aidha
alisema muswada huo unalenga kudhibiti machapisho hadi majarida madogo
na blogs, na kutoa adhabu kali kwa watakaopatikana na makosa, pamoja na
kuyafungia magazeti.
Kwa
upande wa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015, alisema
itaharamisha machapisho ya mtandaoni yanayoonekana na serikali kuwa na
habari za kupotosha, udanganyifu au uongo.
Aidha,
alisema sheria hiyo inatoa mamlaka kwa polisi ya kukagua nyumba za
watuhumiwa, kukamata kompyuta zao na kutaka takwimu zao kutoka kwa watoa
huduma wa mitandaoni
“Itakuwa
ni kosa la jinai kutuma barua pepe au mawasiliano mengine ya
kielektroniki bila ya idhini,” alisema. Kwa upande wa Sheria ya Takwimu
ya Mwaka 2015, Mbowe alisema inaharamisha uchapishaji wa takwimu ambazo
kwa maoni ya serikali zitakuwa ni za uongo, na adhabu yake itakuwa faini
ya Dola 6,000, au hukumu ya miaka mitatu jela.
“Mtafiti au mwandishi anaweza kwenda jela kwa kuchapisha takwimu ambazo serikali haikubaliani nazo,” alisema.
Mbowe
alizitaka nchi washirika katika maendeleo na jumuiya ya kimataifa
kumsisitiza Rais Jakaya Kikwete kutozisaini sheria hizo, na kuzirudisha
tena bungeni ili mambo yote yaliyolenga kuvisambaratisha vyombo vya
habari na kukandamiza uhuru wa kujieleza yawe
No comments:
Post a Comment