Mgogoro Burundi: Upinzani waipinga Tume ya Uchaguzi

Vurugu kumpinga Rais wa Nkurunziza zaendela nchini Burundi.
Vurugu kumpinga Rais wa Nkurunziza zaendela nchini Burundi.
Vyama vya upinzani nchini Burundi vimelikataa pendekezo la tume ya uchaguzi ya nchi hiyo ya kutaka uchaguzi wa rais ufanyike tarehe 15 ya mwezi ujao wa Julai. Mrengo wa upinzani umesema matakwa yao ya kufanyika uchaguzi huru bado hayajatimizwa.
Katibu Mkuu wa chama cha FNL Adolphe Banyikwa amesema maamuzi ya tume ya uchaguzi hayana uhalali kikatiba kwa kutotimiza akidi ya upitishaji maamuzi baada ya wajumbe wake wawili kukimbilia nchini Rwanda wakihofia usalama wa maisha yao.
Aidha upinzani nchini Burundi umetaka mpatanishi wa Umoja wa Mataifa Said Djinnit ajiuzulu kwa kushindwa kuushughulikia mgogoro wa nchi hiyo. Uamuzi wa tume ya uchaguzi ya Burundi wa kusogeza mbele tarehe ya uchaguzi wa rais kutoka Juni 26 hadi Julai 15 umepuuza hata wito wa viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambao walitaka uchaguzi huo usogezwe mbele kwa muda wa angalau wiki sita.
Awali mrengo wa upinzani unaojumuisha vyama 17 ulitoa taarifa ukieleza kuwa uko tayari kwa mazungumzo lakini umeendelea kumtaka  Rais Pierre Nkuruziza aache msimamo wake wa kugombea urais kwa muhula wa tatu. Charles Nditije, mmoja wa viongozi wa upinzani aidha amesema wanataka iundwe tume mp
Umoja wa Mataifa kupitia Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu Zeid Ra’ad Al Hussein ukitahadharisha kuwa Burundi iko kwenye hatari ya kutumbukia tena kwenye lindi la vita vya wenyewe kwa wenyewe.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved