Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha zoezi la uandikishaji jijini
Dar es salaa pamoja na mkoa wa Pwani kwa kutumia mashine za BVR
lililokuwa linategemewa kuanza rasmi tarehe 4.7.2015 jijini Dar es
salaam na 25.06.205 kwa mkoa wa Pwani.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo Habari, NEC imesema imeahirisha
zoezi hilo kutokana na kuchelewa vifa vya uboreshaji kutoka mikoani
ambako zoezi hilo linaendelea pamoja na vifaa vilivyokuwa vinakusudiwa
kuanza kutumia Dar es salaam kupelekwa katika mikoa ambayo wananchi
wamejitokeza kwa idadi kubwa kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la
wapiga kura.
Hata hivyo tume hiyo imewataka wananchi kuwa watulivu wakati vifaa vikisubiriwa kutoka mikoani.
No comments:
Post a Comment