TAMASHA LA MICHEZO, AFYA KUFANYIKA JUNI 14 LEADERS JIJINI DAR

Mratibu wa tamasha hilo, Dimo Debwe Mitiki (katikati) na  Meneja wa Benki ya CRDB Bank ambao ndiyo wadhamini wa tamasha hilo, Leevan Maro (kushoto) na mratibu wa tamasha hilo, Josephine  Kayombo Mratibu  pia wa tamasha hilo.
Sehemu ya wanahabari wakifuatilia tukio.
Rais wa shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja
TAMASHA la michezo na afya lenye lengo la kuboresha afya ambalo limeandaliwa na kampuni ya Fern (T) Ltd linalotarajiwa kufanyika juni 14 katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam,  mratibu wa tamasha hilo, Dimo Debwe  Mitiki,  amesema kuwa lengo kubwa la tamasha hilo ni kuwakutanisha watu wa rika mbalimbali ili kufurahia na kuweka miili yao sawa kwa afya bora.
Amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na burudani kwa ajili ya kuwaburudisha watu na wataalamu mbalimbali waliobobea kwenye sekta ya ufundishaji juu ya ufanyaji mazoezi na wataalamu wa afya watakuwepoa kwa ajili ya kutoa ushauri wa afya na lishe.
Dimo aliongeza kuwa Kampuni ya Fern imetambua na kuona kuwa ni vyema kuandaa tamasha hilo ili watu wengi wajitokeze kwa ajili ya kurekebisha afya zao na akasema kuwa siku hiyo kutakuwa na washiriki kama vile Jogging Club zaidi ya miamoja kutoka wilaya tatu za mkoa wa Dar es Salaam, makampuni na taasisi wakiwemo, CRDB Bank, TCDC, SMART TELECOMMUNICATION  na PSI.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved