SHINDANO LA KUSAKA VIPAJI LA TMT JIJINI DAR LAZIDI KUNOGA

Washiriki wa shindano la kutafuta vipaji (TMT) wakifurahia.
Baadhi ya washiriki wa shindano la TMT wakiigiza.
Picha ya pamoja ya washiriki wa shindano (TMT) na jaji  Haji Salum 'Mboto' aliye mbele yao.

SHINDANO la kusaka vipaji vya wacheza filamu lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT). limezidi kunoga jijini Dar es Salaam kufuatia wingi wa watu zaidi ya 1,000 wakiwemo wazee vijana na watoto kujitokeza kwa wingi katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, katikati ya jiji la Dar es Salaam mapema leo huku.
Akiongea na mwandishi wetu, Meneja mradi wa TMT, Saul Mpock alisema jana ilikuwa ni hatua ya pili ya kusoma ‘Script’ kwa makundi mawili, washindi wakiendelea kubaki huku walioshindwa wakitolewa kwenye mashindano hayo.
Alisema kundi lililobaki litasoma script yake leo huku mchujo ukiendelea na kwamba washindi wa jana na leo wataungana kwa hatua ya tatu.
Mwaka jana mshindi wa shindano hilo, Mwanaafa Mwinzago kutoka Mkoa wa Mtwara alijinyakulia kitita cha shilingi milioni 50 hali inayoleta ushindani mkubwa katika shindano la mwaka huu.
Shindano hilo linaloendeshwa chini ya majaji watatu ambao ni Rich, Monalisa na Roy, jumla ya washindi kumi walipatikana ambao walishiriki kwa mafanikio filamu ya Mpango Mbaya. 

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved