Vijana waanzisha klabu kusaidia kukabili uhalifu


VIJANA zaidi ya 100 kutoka shule za sekondari za mjini Dodoma kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wamepaza sauti zao kupinga vitendo vya kiuhalifu.
Vijana hao wamewataka wenzao kutojihusisha na vitendo vya kigaidi pamoja na matumizi ya dawa za kulevya.
Walisema huku asilimia 31 ya watu nchi ni vijana baadhi yao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya kiuhalifu huku wanafunzi wakishindwa kufanya vizuri shuleni kutokana na matumizi ya dawa za kulevya.
Vijana hao ambao wamejiunga katika klabu ya marafiki wa Jeshi la Polisi kwamba wameamua kujiunga ili kuwa kufichua wahalifu.
Diana Alexander alisema katika elimu waliyopatiwa na Jeshi la Polisi wamejifunza mbinu mbalimbali za kugundua uhalifu unaofanyika ndani ya jamii, pia watahakikisha wanatoa elimu jinsi ya kushiriki katika ulinzi shirikishi kwa vijana wenzao ambao wapo vijiweni.
“Klabu Marafiki wa Jeshi la Polisi imetuwezesha kujifunza elimu mbalimbali ya kuepukana na maovu, na jinsi ya kushiriki katika masuala ya kijamii kama vile ufanyaji wa usafi kwenye maeneo tofauti yanayogusa jamii pia na jinsi ya kupambana na vitendo viovyo,” alisema.
Mratibu wa Klabu Marafiki wa Jeshi la Polisi Dodoma mjini, Afande Ramadhan Mambea alisema wanafunzi hao wameweza kujengewa misingi imara ya ukakamavu ikiwa na elimu ya kuchukia uhalifu na wanaendelea kutoa mafunzo kwa vijana hao ili kukabiliana na uhalifu.
Mambea ambaye pia ni Mkaguzi wa Polisi Tarafa ya Dodoma mjini alisema klabu marafiki wa jeshi hilo la polisi pia wapo kwenye vyuo vya elimu ya juu na katika shule za msingi ambapo kwa pamoja wamekuwa wakifundishwa elimu mbalimbali ikiwemo ya kuchukia uhalifu.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved