Wanafunzi SHINYANGA wakabiliwa na uhaba wa chakula |
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi BUHANGIJA PETER FRANCIS amesema shule hiyo inapewa bajeti ya chakula kutoka serikalini kwa ajili ya wanafunzi 40 wenye ulemavu huku ikiwa na wanafunzi 396 wenye mahitaji maalum.
Ongezeko hilo ambalo limesababishwa na wimbi la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi limesababisha shule hiyo kukabiliwa na changamoto lukuki kubwa ikiwa ni uhaba wa chakula
Changamoto hizo zimeulazimu uongozi wa Shule ya Msingi Maalum ya BUHANGIJA kuomba msaada wa hali na mali kutoka kwa wasamaria wema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi -CCM Mkoa wa SHINYANGA HAMISI MGEJA ametoa wito kwa serikali kutatua matatizo yanayoikabili shule hiyo.
No comments:
Post a Comment