MABINGWA
wa Kandanda Tanzania bara, Young Africans asubuhi hii wanaanza mazoezi
kujiandaa na ligi kuu soka Tanzania bara pamoja na michuano ya klabu
bingwa Afrika mashariki na kati, Maarufu kama Kombe la Kagame
inayotarajia kuanza kutimua vumbi Julai 11 mwaka huu.
Kocha
mkuu wa Yanga aliyerejea nchini usiku wa kuamkia jana, Hans van der
Pluijm analazimika kuanza mazoezi mdogo-mdogo na wachezaji wachache
kwani wengi wapo timu zao za Taifa.
Pluijm
anaanza kuwanoa vijana wake leo uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es
salaam na kufikia Juni 16 mwaka huu wachezaji wote watakuwa wameripoti,
ingawa Kpah Sherman raia wa Liberia anatua leo nchini.
Wakati
huo huo, Yanga inasubiri Baraka za TFF kuhusu idadi ya wachezaji 10 wa
Kigeni aliopendekeza wasajiliwe kuelekea msimu ujao, lakini tayari
imeeleza kwamba ina majina yote ya wanandinga inaowataka.
“Wachezaji
wa Kigeni tumeshawapata, tunachosubiri ni TFF kutangaza idadi
tunayoruhusiwa kusajili. Tuliomba idadi iongezwe kutoka watano wa sasa
mpaka kufikia 10, wakitoa Baraka zao, basi tutatangaza wachezaji
tuliozungumza nao na imebaki kuwasainisha tu”. Amesema katibu mkuu wa
Yanga, Dr. Jonas Tiboroha.(VICTOR)
No comments:
Post a Comment