Kwenye hii post tumeipata benki kuu ya Tanzania ambayo iko tayari
kuzungumzia ishu ya sarafu mpya ya shilingi mia tano kutoonekana sana
kwenye mzunguko wa fedha nchini Tanzania.
‘Benki kuu iliamua kubadilisha kutoka noti na kuleta sarafu ya
shilingi mia tano baada ya kuona noti hiyo inakuwemo kwenye mzunguko kwa
muda mrefu kuliko inavyotakiwa bila kurudishwa Benki hivyo inachakaa
mno’
‘Katika zoezi hilo la kuibadilisha
noti ya shilingi mia tano kuwa sarafu, utakuta kwamba Benki kuu sehemu
sehemu ambayo inaanza usambazaji ni kwamba wanatoa pesa kwa benki za
biashara na zinapokuja huwa tunawatolea wachukue sarafu na noti lakini
kwenye kipindi hiki benki hizi zimekua hazichukui sana sarafu ya
shilingi mia tano kama zinavyochukua noti, ila sarafu hii ipo kabisa‘
No comments:
Post a Comment