BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro limeendelea
kusimamia uboreshaji mazingira kwa kuwatoza faini wafanyabiashara
wasiofuata utaratibu wa usafi kwa kuwafikisha mahakamani.
Hatua hiyo inatokana na kuwepo ugonjwa wa kipindupindu tangu Augosti
mwaka jana, ambapo hadi Februari 14, mwaka huu watu 10 walipoteza
maisha.
Meya wa Manispaa ya Morogoro, Pascal Kihanga alisema hayo juzi,
wakati akiwasilisha mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2016/2017 katika
kikao cha bajeti cha baraza hilo.
Alisema, halmashauri hiyo ilipata kipindupindu Agosti hadi Oktoba
mwaka jana, ambapo wagonjwa 117 walitambuliwa na wengine wawili
walipoteza maisha hadi ulipodhibitiwa.
“Mlipuko wa kwanza ulidhibitiwa kwa kufanya usafi, kutoa elimu ya
afya na kuhamasisha matumizi ya dawa za kutakasa maji,” alisema Meya
huyo.
Pamoja na juhudi hizo, alisema ugonjwa huo ulianza tena Desemba 23
mwaka 2015 kwa mara ya pili, wakati wa sikukuu za Idd na Krismasi na
kusababisha idadi ya wagonjwa na vifo kuongezeka.
No comments:
Post a Comment