Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Joseph Magufuli ameidhinisha kuanzishwa kwa mkoa mpya wa Songwe na wilaya nyingine mpya nchini
Akitoa
tamko hilo kwa niaba ya Rais Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe George Simbachawene amesema kwa
mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977
imempa Mamlaka Rais ya kugawa Nchi kwa kadri ambavyo atakapoona inafaa.
Mhe
George Simachawene amesema kutokana na mamlaka hayo aliyopewa Rais
jumla ya Wilaya sita na Mkoa mmoja wa Songwe umeanzishwa kwa mujibu wa
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Mkoa mpya wa
Songwe umeanzishwa kutoka Mkoa wa Mbeya.
Amezitaja
Wilaya mpya zilizoanzishwa kuwa ni Wilaya ya Songwe Mkoa wa
Songwe,Wilaya ya Ubungo Mkoa wa Dar es salaam, Wilaya ya Kibiti Mkoa wa
Pwani, Wilaya ya Kigamboni Dar es salaam, Wilaya ya Mlanyi Mkoa wa
Morogoro na Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi
“
Nichukue fursa hii kuwaagiza Wakuu wa Mikoa wote ambao Wilaya mpya
zimeanzishwa kufanya maandalizi rasmi ili Mkoa na Wilaya hizo ziweze
kuanza kufanya kazi,aidha mkazo uwekwe kwenye upatikanaji wa Ofisi na
huduma zote muhimu kupatikana kwa urahisi katika Mkoa naWilaya hizo
mpya” Alisema Mhe Simbachawene.
No comments:
Post a Comment