SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), leo limeamua
kuwa, mchezaji Ramadhani Yahya Singano 'Messi' ni huru na sasa anaweza
kujiunga na timu yoyote.
Taarifa kutoka kwenye kikao cha Kamati ya Sheria Maadili na Hadhi za
Wachezaji ya TFF kilichofanyika leo, imesema kwamba Simba SC walishindwa
kutekeleza baadhi ya vipengele vya Mkataba, hivyo wanapoteza haki za
kummiliki mchezaji huyo.
Chini ya Mwenyekiti wake, Richard Sinamtwa, Kamati hiyo imejiridhisha
Messi hakuwahi kupewa nyuma ya kuishi na Simba SC jambo ambalo ni
kinyume cha Mkataba baina yake na klabu hiyo.
Simba SC iliwakilishwa
na Mwenyekiti wake wa Kamati yake ya Usajili, Zacharia Hans Poppe na
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Collins Frisch wakati Messi alifika na
Mwenyekiti wa Chama cha Wachezaji Tanzania (SPUTANZA), Mussa Kisoky.
Maamuzi haya ni faraja kwa Messi ambaye anahusishwa kwa kiasi kikubwa
na kuhamia Azam FC. Messi aliyeibukia timu ya vijana ya Simba SC miaka
minne iliyopita, hivi karibuni ameibua shutuma dhidi ya klabu yake hiyo
kwamba imeghushi Mkataba wake. Messi anadai Mkataba wake halali ulikuwa
unamalizika mwaka huu, na si huu wa sasa ambao inaelezwa utamalizika
mwakani.
Lakini Simba SC imeendelea kusistiza mchezaji huyo alikuwa ana
Mkataba wa miaka mitatu. Awali, Sekretarieti ya TFF, chini ya Katibu
wake, Selestine Mwesigwa ilizikutanisha pande zote mbili, mchezaji na
Simba SC na kuamuru waketi chini na kutayarisha Mkataba mpya baada ya
kuona huu wa sasa una mushkeli. Hata hivyo, Messi akakataa na kuamua
kulihamishaia suala hilo Kamati ya Sheria ambayo leo imempa kile
alichotaka ‘kuwa mchezaji huru’.
Safari FIFA?; Hans Poppe amesema kwamba watakwenda mbele kusaka haki zao
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Hans Poppe amesema kuwa,
baada ya matokeo hayo, wanakwenda kukutana ili kujua hatua zaidi za
kuchukua, lakini dhahiri hawataishia hapo.
“Tuliwasilisha ushahidi
wote mbele ya Kamati, tumeonyesha mshahara wake ulikuwa kiasi gani na
tumeonyesha kwa nini alikuwa anapewa laki moja (100,000) zaidi.
Ili akalipie kodi ya nyumba, lakini bado hatukueleweka. Tunaamini
hapa si mwisho, vipo vyombo vingine ambavyo vitatupa haki yetu,
tunakwenda kukutana kuangalia uwezekano wa kulipeleka suala hili
huko,”amesema Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ).
KASEJA AINGIA ‘DARASANI’ KUSOMEA UKOCHA WA MAKIPA...
KIPA
wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Juma Kaseja Juma ni miongoni mwa
watakaoshiriki kozi ya makocha wa makipa nchini itakayofanyika Julai 13
hasi 17 mwaka huu mjini Dar es Salaam.
Kaseja amewika timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na klabu zote kubwa nchini Simba na Yanga SC na kwa sasa japo hajatangaza kustaafu soka, lakini ameanza kupata mafunzo ya ukocha.
Katikati ya msimu uliopita aliomba mwenyewe kujitoa Yanga SC akidai klabu hiyo ilishindwa kutekeleza vipengele vya Mkataba baina yao na tangu hapo amekuwa akifanya mazoezi na timu ya makipa nchini.Kozi hiyo inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), itashirikisha jumla ya makocha wa makipa 29 wa klabu za Ligi Kuu na timu za taifa na itafanyika katika ofisi za TFF zilizopo Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam.
Mbani na Kaseja, wengine ni Juma Nassor Pondamali, kocha wa makipa wa klabu bingwa Tanzania Bara, Yanga SC, Rafael Mpangala (Mgambo JKT), Adam Abdallah Moshi (Simba SC ), Khalid Adam Munnisson (Mwadui FC), Choke Abeid (Toto African), Mussa Mbaya (Ndanda FC), Idd Abubakar Mwinchumu (Azam FC), Herry Boimanda Mensady (Tanzania Prisons), Kalama Ben Lwanga (Stand United) na Patrick Mwangata (Mtibwa Sugar).
Wengine ni Abdi Said Mgude (Coastal Union), Razack Siwwa (African Sports Tanga), Josia Steven Kasasi (Mbeya City), Ramadhani Juma (Kagera Sugar Kagera), Abdallah Said Ngachimwa (JKT Ruvu), John Bosco (Majimaji FC Ruvuma), Fatuma Omary (Twiga Stars), Juma Kaseja Juma (Huru), Athuman Mfaume Samata (Ilala) na Peter Manyika John (Taifa Stars).
Hussein Tade Katadula (African Lyon), Juma Mohamed Bomba (Kinondoni), Mwameja Mohamed Mwameja (Ilala), Agustino Malindi Mwanga (Kigoma), Mohamed Abbas Silima (Police SC. Zanzibar), Bakari Ali Kilambo (Kizimbani SC Zanzibar), Hafidh Muhidin Mcha (Zanzibar Heroes), Elyutery Deodatusy Mholery (Kinondoni), Salim Waziri (Tanga)..

Nkurunzinza kortini Arusha
RAIS wa Burundi, Pierre Nkurunziza ameshitakiwa katika Mahakama ya
Afrika Mashariki iliyopo jijini Arusha kutokana na hatua yake inayotajwa
kukiuka Katiba ya nchi hiyo kwa kuwania kipindi cha tatu cha Urais.
Kesi hiyo, ambayo pia inamjumuisha Mwanasheria Mkuu wa Burundi, Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi kwa nchi ya Burundi pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mujibu wa taarifa maalum kutoka kwenye taasisi ya mawakili wa Kanda ya Afrika (PALU) inayosimamia shauri hilo.
Hii sasa inamaanisha kuwa kiongozi huyo wa Burundi atahitajika wakati wowote kwenda Arusha mahakamani, kuhudhuria kesi yake.
Ripoti hiyo iliyoidhinishwa na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha PALU, Jancelline Amsi, imeeleza kuwa shauri hilo namba RCCB 303 la 2015 dhidi ya Nkurunziza liliwasilishwa katika Mahakama ya Jumuiya na Umoja wa mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka nchi za Kenya, Rwanda, Uganda, Burundi na Tanzania chini ya mwamvuli wa taasisi yao ya ‘East African Civil Society Organizations’ Forum (EACSOF).’
Mashirika hayo yanamtuhumu Rais Nkurunziza kwa kukiuka katiba ya nchi yake pamoja na kuvunja makubaliano ya Amani ya Arusha katika dhamira yake ya kugombea urais kwa kipindi cha tatu, hatua ambayo imesababisha machafuko nchini Burundi yaliyopelekea vifo vya wananchi wapatao 70 huku wengine zaidi ya 140,000 wakiikimbia nchi yao.
Hatua hiyo inakuja wakati Rais Nkurunziza akiwa amejikita katika kampeni za urais, hivyo kushindwa kujumuika na wakuu wa nchi za EAC wanaokutana Dar es Salaam kujaribu kutafuta ufumbuzi wa tatizo la kisiasa la Burundi.
Msemaji wa Rais Nkurunziza, Gervais Abahiro alieleza kutoka Bujumbura alisema kuwa bosi wake huyo angewasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Alain Aime Nyamit

Yanga yageukia Polisi
MABINGWA wa soka wa Tanzania Bara, Yanga watacheza na Kombaini ya
Polisi Tanzania katika mechi ya kirafiki itakayofanyika kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam, Jumamosi wiki hii.
Mechi hiyo ni kwa ajili ya kujiweka sawa kwa mashindano yanayozikabili timu hizo mbili ambapo Yanga inajiandaa kushiriki Kombe la Kagame litakaloanza Dar es Salaam, Julai 18, mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi jana kwa vyombo vya habari, Kombaini ya Polisi itashiriki katika michezo ya Umoja wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) itakayoanza mwishoni mwa mwezi huu nchini Swaziland.
Akizungumza jana Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Michezo wa Jeshi la Polisi, Jonas Mahanga alisema kikosi cha Polisi kitatumia mchezo huo kubaini upungufu na kuufanyia marekebisho kabla ya kuelekea Swaziland ambapo alisema taratibu zote zimeshakamilika.
Mahanga alisema mchezo huo utakuwa mzuri na wa kuvutia kutokana na wachezaji wanaounda Kombaini ya Polisi kuonesha kiwango kikubwa katika kambi yao inayoendelea katika Chuo cha Taaluma ya Polisi (DPA) kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam.
Alisema Kombaini ya Polisi inaundwa na wachezaji askari kutoka timu za Polisi za Tanzania Bara na Zanzibar ambapo wengi wa wachezaji hao ni wale waliokuwa wanacheza Ligi Kuu zao pamoja na Ligi Daraja la Kwanza.
Aidha, Mahanga alisema kwa upande wa netiboli, nayo itacheza mchezo wa kirafiki na Kombaini ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ili kuhakikisha kuwa inafanya vizuri nchini Swaziland na kurudi na ubingwa.
Alisema kwa ujumla timu zote zinazojiandaa na michezo hiyo zinaendelea vizuri ambapo wanariadha waliokuwa katika kambi ya Taifa mkoani Manyara wiki hii wataungana na wenzao ili kufanya mazoezi kwa pamoja.
Alisema lengo la michezo hiyo ya SARPCCO ni kujenga mahusiano miongoni mwa askari Polisi wa nchi za kusini mwa Afrika pamoja na kubadilishana mbinu za kukabiliana na uhalifu ambapo Polisi Tanzania itashiriki katika mchezo wa mpira wa miguu, netiboli, riadha na vishale.

Wezi Mfuko wa Mafuta, Gesi kuozea jela
BUNGE limepitisha miswada miwili iliyokuwa imesalia ya mafuta na gesi
ambapo watakaobainika kuchota fedha katika Mfuko wa Mafuta na Gesi
utakaoanzishwa watapewa adhabu mbalimbali ikiwemo kifungo cha miaka 30
jela au kufilisiwa mali zao.
Hata hivyo, wabunge wa upinzani wamemtaka Rais Jakaya Kikwete wakimuomba asisaini miswada hiyo, huku pia wakitangaza kususia vikao vyote vilivyobaki vya Mkutano wa 20 wa Bunge, ambalo linatarajiwa kumaliza uhai wake Alhamisi wiki hii kwa Rais Kikwete kuhutubia.
Akizungumza bungeni jana wakati akifanya majumuisho kwa kujibu hoja za wabunge mbalimbali waliochangia Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi wa Mwaka 2015, Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima alisema muswada umeweka adhabu kali kwa watakaobainika kutumia fedha za mfuko huo.
Alizitaja adhabu hizo kuwa ni faini isiyopungua kiasi ambacho mhusika amechukua, au kifungo cha miaka 30 jela au vyote viwili kwa pamoja na kuongeza kuwa pia sheria inampa hakimu uwezo wa kutoa adhabu ya kumfilisi mhusika na kesi hiyo itakuwa ya uhujumu uchumi.
Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi wa Mwaka 2015, unaweka masharti kuhusu uanzishwaji wa Mfuko wa Mafuta na Gesi ambao utakuwa na Akaunti mbili zitakazotunzwa na kusimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania.
Akaunti hizo ni Akaunti ya Kupokea Mapato na Akaunti ya Kutunza Mapato. Muswada mwingine uliopitishwa jana ni Muswada wa Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uchimbaji Tanzania wa Mwaka 2015, ambapo wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge waliochangia, Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, alisema unalenga kuondoa changamoto mbalimbali zilizojitokeza kwenye sera, sheria na miongozo mbalimbali ambayo ilikuwepo kwa muda mrefu ili kuleta ufanisi bora zaidi katika sekta ya gesi asilia.
Pamoja na mambo mengine, muswada huo unaanzisha taasisi tatu mpya ambazo ni Ofisi ya Ushauri Kuhusu Petroli na Gesi chini ya Ofisi ya Rais, Kampuni ya Mafuta ya Taifa na Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA). Pia unaweka uwazi katika leseni na mikataba ya madini, gesi na mafuta.
Muswada huo ulipitishwa na wabunge wengi wa CCM, huku wa upinzani wakiwa wanne tu, ambao ni Philipa Mturano na Leticia Nyerere (Viti Maalumu Chadema) na wawili wa CUF, Said Suleiman Said (Mtambwe) na Hamad Rashid Mohammed (Wawi).
Akizungumza baada ya Bunge kupitisha miswada hiyo kwa nyakati tofauti jana, Spika wa Bunge, aliwapongeza wabunge kwa michango yao katika kuiboresha na kwamba sasa wanasubiri Rais Kikwete aisaini iwe sheria.
Muswada wa Sheria ya Petroli wa Mwaka 2015 wenyewe ulipitishwa juzi. Wakati huohuo, akizungumza na waandishi wa habari hotelini mjini hapa jana, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni, Freeman Mbowe, alisema wanaomba Rais Kikwete asisaini miswada hiyo, ambayo iliwasilishwa kwa pamoja bungeni Jumamosi.
Pia alisema wabunge wote wa upinzani hawatahudhuria vikao vyote vilivyobaki vya Bunge ikiwa ni pamoja na kile cha Alhamisi, ambapo Rais Kikwete atahutubia Bunge ikiwa ni hatua mojawapo ya kuhitimisha uhai wa miaka mitano wa bunge hilo.
Alisema wabunge wote hao ambao wanatoka vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi NLD vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) walitarajiwa kuondoka Dodoma jana kurejea Dar es Salaam kwa ajili ya vikao zaidi kwenye vyama vyao na baada ya kesho watazungumza hatua itakayofuata.

Okwi apelekwa Denmark
MSHAMBULIAJI nyota wa Uganda, Emmanuel Okwi ana nafasi nzuri ya kuula
endapo atafanikiwa kufanya vizuri katika majaribio nchini Denmark mwezi
huu.
Okwi anayechezea Simba, anatarajiwa kwenda nchini Denmark kufanya majaribio katika Klabu ya Sonderjyske inayoshiriki Ligi Kuu ya huko kuanzia kesho.
Kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa kwenye tovuti ya Klabu ya Simba jana, majaribio hayo yatakuwa ya siku 14 kuanzia kesho na baada ya hapo klabu hiyo ya Sonderjyske itatuma ripoti kamili ya majaribio hayo.
Rais wa Simba, Evans Aveva alisema: “Simba inafurahi sana kuona wachezaji wake wanapata nafasi hizi za kuonesha vipaji vyao tena kwenye viwango vya kimataifa zaidi, hivyo Simba inamtakia kila la kheri Okwi kwenye majaribio yake ya siku 14 kwenye Klabu ya Sonderjyske iliyopo kwenye ligi ya Denmark.”
Okwi aliyezaliwa miaka 23 iliyopita nchini Uganda, aliwahi pia kucheza kwa muda mfupi katika Klabu ya Etoile Sportive du Sahel ya Tunisia na baadaye kuichezea Yanga kabla ya msimu uliopita kurudi klabu yake ya Simba.
Katika hatua nyingine, mshambuliaji na nahodha wa Azam FC, John Bocco mambo yake yamemnyookea baada ya Klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini kukubali kumsajili.
Taarifa zilizopatikana kutoka vyanzo mbalimbali vya habari, Azam FC imekubali kumuuza mchezaji huyo na kinachosubiriwa ni timu hiyo kumalizana juu ya maslahi binafsi ili kuhamia katika timu hiyo.
Kwa mujibu wa mtandao wa bongostaz, Azam FC imekubali kumuuza mshambuliaji huyo kwa kitita cha Dola za Marekani 80,000 ikiwa ni sawa na zaidi ya Sh milioni 160,000 kwa klabu hiyo.
Na sasa kinachosubiriwa na Free State kumalizana na mchezaji juu ya maslahi binafsi ili mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Tanzania, ahamie Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini.
Mshambuliaji mahiri, Mrisho Ngassa aliyesajiliwa na Free State miezi miwili iliyopita baada ya kumaliza mkataba Yanga, anaeleza kuwa ndiye aliyempa ulaji huo Bocco kwa kuwapa viongozi wa timu hiyo mawasiliano ya Bocco.
Hata hivyo, gazeti hili lilipomtafuta Msemaji wa Azam FC, Jaffari Idd kuzungumzia taarifa hizo, alisema hazina ukweli na kama zitakuwa na ukweli zitawekwa mara moja katika tovuti ya klabu hiyo.
Bocco aliwahi kufanya majaribio Afrika Kusini katika Klabu ya Supersport na Algeria na kufuzu ila hakuuzwa kutokana na dau dogo

Subscribe to:
Posts (Atom)