Burundi upinzani wasaema uchaguzi hauwezekani kwa sasa
Vyama vikuu vya upinzani nchini Burundi vimesema "haiwezekani" kuitisha
wiki ijayo uchaguzi huru na wa haki na kwamba matokeo yake hayastahiki
kutambuliwa pindi ukiitishwa. Vyama hivyo vikuu vya upinzani vinasema
kuendelea na maandalizi ya uchaguzi licha ya machafuko yaliyoenea mji
mkuu ni sawa na kuuteka nyara uchaguzi huo.Taarifa ya vyama hivyo vya
upinzani imetolewa baada ya mpinzani mwengine wa mhula wa tatu wa rais
Pierre Nkurunziza kuuliwa na wengine wawili kujeruhiwa kusini mwa nchi
hiyo.Wanaharakati wanalalamika wakisema wanazidi kushambuliwa na wafuasi
wa wa chama tawala CNDD-FDD."Katika taarifa hiyo vyama vikuu vya
upinzani vinamtuhumu rais Nkurunziza na chama tawala kuvifumba mdomo
vyombo huru vya habari,kuwashikilia jela wapinzani na kusababisha wimbi
kubwa la wakimbizi.Uchaguzi wa bunge umepangwa kuitishwa juni tano ijayo
na ule wa rais juni 26.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment