“Uhalifu waliofanya askari wa kigeni CAR uchunguzwe”
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ametaka ufanyike
uchunguzi zaidi kuhusu utumiaji mbaya wa kijinsia uliofanywa na askari
wa nchi tofauti za kigeni dhidi ya watoto katika Jamhuri ya Afrika ya
Kati. Zeid Ra'ad Al Hussein amesema leo kuwa baada ya kutolewa ripoti
kuhusiana na utumiaji mbaya wa kijinsia waliofanyiwa watoto nchini humo
na askari wa kulinda amani wa Ufaransa, nchi nyingine nyingi zimetakiwa
zifanyiwe uchunguzi juu ya madai yalioyotolewa ya utumiaji mbaya wa
kijinsia na mauaji ya watu wasio na hatia yaliyofanywa na askari wa nchi
hizo wanaolinda amani chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa. Imeelezwa
kwamba zimetolewa tuhuma nzito dhidi ya askari wa nchi nyengine pia
zikiwemo za mauaji, utekaji nyara na utumiaji mbaya wa kijinsia. Kwa
mujibu wa Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa mbali na
askari wa Ufaransa, kuna ripoti zinazohusisha askari wa nchi nyengine
pia waliohusika na utumiaji mbaya wa kijinsia. Mwishoni mwa mwezi
uliopita wa Aprili, gazeti la The Guardian liliripoti kuwa katika
kipindi cha kati ya Disemba mwaka 2013 hadi Juni 2014 wakati wa
operesheni ya kijeshi katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati,
Bangui askari wa Ufaransa waliokuwa wametumwa nchini humo waliwafanyia
vitendo vichafu vya kuwabaka na kuwalawiti watoto wadogo wa kiume wenye
umri hata wa miaka tisa ili kuwagaia pesa na chakula…/
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment