Viongozi wanne wa upinzani nchini Senegal, ambao awali walitiwa
mbaroni na kufungwa jela kwa ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma,
waliachiliwa huru hapo jana Ijumaa. Aïda Ndiongue mpinzani maarufu wa
serikali ambaye amekuwa jela kwa kipindi cha miezi 18 kwa tuhuma za
kuichafulia jina serikali na ufisadi, aliachiliwa huru jana kwa amri ya
mahakama ya nchi hiyo. Wapambe wake watatu, ni miongoni mwa watu
walioachiliwa huru kutoka jela. Wizara ya Sheria nchini Senegal jana
ilitangaza kuwa, imelifanyia uchunguzi ombi la kuangaliwa upya faili
hilo, ombi ambalo lilitolewa na watuhumiwa. Aïda Ndiongue ni
mfanyabiashara mashuhuri wa nchi hiyo na kiongozi mwandamizi wa chama
cha Democrasia, ambacho ni chama kikuu cha upinzani. Mwanasiasa huyo,
anatuhumiwa kwa kufuja fedha za serikali zilizokuwa zimetolewa kwa ajili
ya ujenzi wa idara za serikali na kupambana na mafuriko na makazi duni,
katika kipindi cha Rais Abdoulaye Wade. Mtuhumiwa mwingine wa ufusadi
ni Karim Wade mwanaye Abdullahi Wade, rais wa zamani wa Senegal ambaye
baada ya baba yake kushindwa katika uchaguzi, alitiwa mbaroni na
kufungwa jela kitendo ambacho kiliibua uhasama mkubwa baina ya Wade na
rais wa sasa Macky Sall.Bottom of Form
Top of Form
Bottom of Form
No comments:
Post a Comment