Jaji mstaafu Damian Lubuva |
“Vyama vya siasa visichukulie wanafunzi kama ajenda ya kupata kura katika Uchaguzi wa Mkuu wa Oktoba, lazima waangalie sheria na kanuni zinasemaje,” alisema.
Alisema hayo jana wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari mjini hapa kuwa wanasiasa wamekuwa wakihoji wanafunzi kujiandikisha vyuoni huku wakati wa uchaguzi wakiwa likizo mbali na vyuo.
Alisema Tume haitaweza kuweka utaratibu maalum kwa ajili ya wanafunzi tu na kuwataka viongozi wa kisiasa kuacha Tume kufanya kazi yake kwani kumekuwa na upotoshaji mkubwa .
Hilo linakuja kufuatia kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa ya kuitaka Tume kutoa tamko juu ya wanafunzi wanaojiandikisha wakiwa vyuoni watapiga kura wapi wakati wa uchaguzi ambapo watakuwa likizo nyumbani kwao mbali na vyuo.
No comments:
Post a Comment