#NYAYOZAKTMA2015 bado inakukutanisha na wadau mbalimbali wa tuzo hizi wakiwemo washiriki wenyewe, waandaaji na mashabiki wakitoa maoni yao tofauti tofauti kuhusiana na tuzo hizi za KTMA 2015.
Makomando ni kundi ambalo limeingi katika kugombea tuzo ya “Kikundi Bora Cha Mwaka Bongo Flava” ambapo wanashindana na Weusi, Yamoto Band, Navikenzo na B.O.B.
Makomando wanasema wana uhakika tuzo ni yao, na mwaka huu iko poa sana, iko tofauti ina ushindani mkubwa pia, wao wamewaachia mashabiki wao ndo wamejipanga kuwapigia kura, tuzo ni yao wana uhakika labda litokee lakutokea.
Kitu ambacho kinawafanya wadumu kwa muda mrefu kwa miaka minne, ni kwa sababu wanashirikiana, wanapendana kama kuna tatizo wanaelewana kabla halijatoka hadharani.
No comments:
Post a Comment