WAZIRI wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Samuel Sitta, amesema
ataendelea kudumisha na kulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,
ikiwa atapewa ridhaa ya kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sitta alisema hayo juzi, wakati akiwashukuru wanachama wa CCM wa Wilaya
ya Bunda waliofika kumdhamini ili ateuliwe kuwa mgombea urais, shughuli
iliyofanyika katika kiwanja cha Ofisi ya CCM Wilaya ya Bunda, mkoani
Mara.
Mgombea huyo alisema ataulinda Muungano wa Tanzania na kuendeleza mema
yote ya muungano huo kama ulivyoasisiwa na waasisi ambao ni hayati
Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Karume, kwa manufaa ya pande zote mbili
za nchi yetu.
Kuhusu katiba, alisema atasimamia uboreshaji wa katiba ya wananchi
ambayo tayari imekwisha pitishwa na Bunge Maalumu la Katiba, ambalo yeye
alikuwa mwenyekiti ili kuwapa haki wananchi wanaoishi Tanzania bara na
visiwani.
Alitoa mfano kuwa, Katiba mbaya husababisha umwagaji wa damu na wananchi
kuwa wakimbizi nchini mwao, kama vile Burundi ambako hivi sasa wananchi
wanaikimbia nchi hiyo, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto.
No comments:
Post a Comment