ASELEMAN Jafo, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo |
SELEMAN Jafo, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, amebaini upotevu wa Sh 180 milioni katika halmashauri ya wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma.
Kutokana na kubainika kwa upotevu wa fedha hizo Jafo alitoa
saa 48 kwa Hussein Issa ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Kondoa, kuhakikisha anapeleka maelezo ya kina katika Ofisi ya
TAMISEMI juu ya kuibiwa kwa fedha hizo ambazo ni za walipakodi
watanzania.
Agizo
hilo la Jafo lilitokana ziara ya kikazi iliyofanywa na naibu waziri
huyo sambamba na kufanyika kwa kikao cha ndani katika Halmashauri hiyo.
Alisema,
Serikali ya Awamu ya Tano haitavumilia kiongozi yoyote ambaye atafanya
ubadhilifu kwa fedha ya Umma au jambo lolote ambalo linaonekana kuwepo
na alufu ya ufisadi.
Alisema
nchi imekuwa ikiendeshwa kimazoea na watu kujilimbikizia mali bila kuwa
na hofu ya kuhojiwa jambo ambalo liliwafanya watumishi wa Umma kuwa na
kiburi na kufanya kile wanachofikiria.
“Nchi
imekuwa ikiendeshwa kimazoea sana watu wanakula hela bila utaratibu na
wanafunika funika tu mambo huku wakiwafanya watu kama vipofu, hili
haitavumiliwa hata kidogo lazima hatua stahiki zichukuliwe,” alisema.
Jafo alisema,
anataka maelezo ya kina juu ya wizi wa fedha hizo na ndani ya masaa
hayo 48 anataka awe amepata taarifa pale ofisini kwake.
Sambamba
na hilo, aliagiza watu nane wanaotuhumiwa kuhusika na wizi wa fedha
hizo wasimamishwe kazi na kukaa pembeni kupisha uchunguzi.
Aidha, aliwaagiza
maofisa utumishi na wakuu wa idara kuwajibika na kutekeleza majukumu
yao kikamilifu na kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea.
Naibu wiziri huyo alieleza
kuwa kumekuwepo na malalamiko mengi juu ya watendaji we ngazi ya chini
ambao wamekuwa wakionewa na kutopatiwa haki zao kama inavyostahili.
Alisema, watumishi hao wanalalamika kutolipwa malimbikizo yao mbalimbali kama fedha za likizo na kutopandishwa vyeo kwa wakati.
No comments:
Post a Comment