KITENDAWILI cha kocha atakayeifundisha Simba msimu ujao kinatarajiwa kuteguliwa leo, wakati jina litakapowekwa hadharani.
Simba ilishindwana na kocha wake Mserbia Goran Kopunovic,
aliyeiongoza timu hiyo kumaliza ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu
Tanzania Bara uliomalizika hivi karibuni.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya timu hiyo, Zacharia Hanspoppe
alisema jana kuwa, leo wanatarajia kutangaza jina la kocha huyo baada ya
kushindwana na yule wa awali.
Ilidaiwa kuwa Kopunovic alikuwa akitaka kiasi kikubwa cha fedha ili
kusaini mkataba mpya wa miaka miwili na Simba ilikuwa ikimtaka kocha
huyo kwa miezi tisa.
Awali, kocha huyo alikuwa na mkataba wa miezi sita, uliomalizika Jumapili ya wiki iliyopita baada ya ligi kufikia tamati.
Awali, Simba ilisema kuwa kulikuwa na majina ya makocha sita
waliojitokeza kujaza nafasi ya kocha huyo Mserbia aliyetaka kiasi cha
dola za Marekani 50,000 (ambazo ni sawa na Sh milioni 100) kwa ajili ya
kusaini mkataba.
Pia, kocha huyo inadaiwa alihitaji kiasi cha dola 8,000 kwa ajili ya
mshahara wake wa mwezi, lakini Simba ikashindwa kukubaliana na masharti
hayo ya kocha huyo.
Hatahivyo, Simba haikuwataja makocha hao sita walioomba kibarua cha
kuinoa timu hiyo, ambayo haijashiriki mashindano ya kimataifa kwa misimu
mitatu mfululizo baada ya kushindwa kumaliza ligi ndani ya mbili bora.
Ilielezwa kuwa makocha hao sita wangepunguzwa hadi kufikia wawili,
ambao wangechuana kwa vigezo ili kumrithi kocha huyo aliyemaliza muda
wake.
Simba imesema kuwa iko makini katika mchakato huo wa kusaka kocha ili kuiwezesha timu hiyo kufanya vizuri msimu ujao na
No comments:
Post a Comment