Balozi AMINA SALIM ALI |
Balozi AMINA SALIM ALI ni mmoja wa madaka hao ambaye amezunguka katika mikoa ya MOROGORO NA PWANI kutafuata udhamini wa wanachama wa chama hicho ikiwa ni moja ya masharti ya kupitishwa na chama hicho ambapo ameahidi kuboresha uchumi wa Taifa kwa kutumia maliasili zilizopo nchini.
Akiwa Mkoani MOROGORO BALOZI AMINA SALIM ALI mwanamke pekee ndani ya CCM aliyejitokeza mpaka sasa kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea nafasi ya urais ametembelea tawi la CCM DAKAWA MVUMERO na akiwa Mkoani PWANI ametembelea tawi la KILUVYA kutafuta udhamini wa wanachama wa chama chake kuteuliwa kugombea nafasi ya urais.
Idadi kubwa ya waliojitokeza ni wanawake waliokuwa tayari kumuunga mkono kwa idadi kubwa zaidi ya ile aliyoiomba.
Akiwashukuru wananchi hao BALOZI AMINA amesema iwapo chama chake kitampa ridhaa atahakikisha masuala yanayowahusu wanawake yanapatiwa ufumbuzi kwa haraka kwa kile alichoeleza kuwa masuala ya wanawake ni masuala ya jamii nzima hivyo kuyatatua ni kutatua kero za jamii kwa ujumla.
Kwa mujibu wa sheria za chama cha mapinduzi mgombea urais anatakiwa kujaziwa fomu za udhamini na wanachama 450 kutoka mikoa Kumi Tanzania Bara na Mitatu visiwani Zanzibar.
No comments:
Post a Comment