Aliyejiandikisha mara 2 katika daftari la kudumu akamatwa na polisi


Aliyejiandikisha mara 2 katika daftari la kudumu akamatwa na polisi

Wakati zoezi la Uandikishaji wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura limeingia siku ya Ishirini mkoani Mbeya, Jeshi la polisi wilayani Rungwe linamshikilia mwanafunzi wa kidato cha Nne katika shule ya msingi Kiwira, Vekline mwankenja kwa kujiandikisha mara mbili.

Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mwalimu ZAINAB MBUSSI ameiambia TBC kuwa VEKLINE MWANKENJA amekutwa na shahada mbili ambazo amejiandikisha katika vituo viwili tofauti vya kujiandikisha, vilivyo jirani.

Zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwa kutumia mfumo wa BVR limeendelea mkoani Mbeya tangu limeanza May 19 mwaka huu, na June 28 linatarajiwa kuhitimishwa,pamoja na kuwepo kwa changamoto kadhaa, uvunjaji wa sheria umejitokeza wilayani Rungwe.

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved