Mkuu wa mkoa wa PWANI Mhandisi EVARESTI NDIKILO |
Mhandisi NDIKILO ametoa rai hiyo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili kwa wataalamu kutoka ngazi ya wilaya watakaoratibu zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya kupigiakura mwa mpya wa BVR.
Naye mwenyekiti wa wakurugenzi katika mkoa wa PWANI JENIFA OMOLO amemhakikishia mkuu wa mkoa kuwa halmashauri zote zimejipanga kusimamia vyema zoezi hilo ili kila mtanzania mwenye umri wa kupiga kura awe amejiandikisha bila usumbufu.
Zoezi la uandikishaji katika daftari la kudumu la mpiga kura katika mkoa wa pwani litaanza Rasmi June 14 mwaka huu na litadumu kwa muda wa siku thelathini.
No comments:
Post a Comment