Saïd Djinnit, msuluhishi wa Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Maziwa Makuu.
Na RFI
Vyama 17
vya upinzani nchini Burundi vimesema havina tena imani na mjube maalumu
wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Maziwa Makuu, Said
Djinnit, na kuomba mpatanishi mpya katika Umoja wa Mataifa.
Vyama vya
upinzani nchini Burundi vimemtuhumu mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa
katika ukanda wa maziwa makuu Said Djinnit ambae ni mpatanishi wa
mgogoro wakisiasa uliopo kwa kuegemea upande mmoja na kuomba kuteuliwa
kwa mpatanishi mwingine katika mazungumzo na serikali ya rais Pierre
Nkurunziza.
Vyama
hivyo vinamkosoa Djinnit kuwasilisha ripoti yake kwa marais wa nchi za
jumuiya ya Afrika mashariki mjini Dar es Salaam juma lililopita bila ya
kuwashirikisha kwa kile kilichoandikwa katika ripoti hiyo.(P.T)
No comments:
Post a Comment