Mmiliki ailaumu DAWASA kuvunja jengo lake Mbezi-Makonde


Mmiliki wa jengo moja lilipo Mbezi Makonde Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam ameilalamikia mamlaka ya maji safi na taka Dar es salaam - DAWASA kwa kuvunja nyumba yake ya biashara bila taarifa wala malipo.
Mmiliki yuyo, Zureha Salim amedai kuwa miaka miwili iliyopita DAWASA walihitaji eneo la mbele ya nyumba hiyo kwa ajili ya kupitisha bomba kubwa la maji hatua ambayo hawakukubaliana nayo na kufungua kesi mahakamani na kusimamisha uvunjaji wa jengo hilo hadi pale uamuzi utakapotoka.
Katika hali ya kushangaza majira ya saa 12 jana jioni walifika askari pamoja na watendaji kutoka DAWASA na kuwatoa na kuanza kuvunja jengo hilo huku wao wakidai kuwa kesi yao ilitakiwa kusikilizwa mwezi julai.(P.T)

No comments:

Post a Comment

©2015 New Day Pro Media.All Rights Reserved