Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kebwe (aliyesimama)
akizunguza wakati wa kuhitimisha kampeni dhidi ya maradhi ya Fistula
katika mikoa ya kanda ya kati, mjini Dodoma jana. Waliokaa kutoka
kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans, Mkuu wa Vodacom
Tanzania Kanda ya kati, Mruta Hamisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja
wa Mataifa la UNFPA, Rutasha Dadi. Kampeni hiyo ilikuwa ikiendeshwa na
Hospitali ya CCBRT na Vodacom Foundation ilifanyika katika mikoa mitatu
ikiwa na dhumuni la kutoa elimu kwa Umma na kuwasisitiza wanaume
kuwaruhusu wakinamama kujitokeza ili wakatibiwe maradhi hayo kwani
yanatibika. Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000 kwa mwaka hupatwa
na maradhi hayo wanapojifungua.
Mkuu wa
Vodacom Tanzania Kanda ya kati, Mruta Hamisi ( aliyesimama kulia)
akizungumza wakati wa kuhitimisha kampeni dhidi ya maradhi ya Fistula
iliyofanyika katika mikoa mitatu Nchini na kumalizikia katika mikoa ya
kanda ya kati, mjini Dodoma jana.Waliokaa ni Naibu Waziri wa Afya na
Ustawi wa jamii, Dk Stephen Kebwe (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa
CCBRT, Erwin Telemans.Kampeni hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Hospitali ya
CCBRT na Vodacom Foundation ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa Umma na
kuwasisitiza wanaume kuwaruhusu wakinamama kujitokeza ili wakatibiwe
maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000
kwa mwaka hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.
Wakazi wa
manispaa ya Dodoma wakihudhuria kwa wingi kwenye hitimisho la kampeni
dhidi ya maradhi ya Fistula. Ambapo Naibu Waziri wa Afya Ustawi wa
Jamii, Dk Stephen Kebwe alihitimisha kampeni hizo katika viwanja vya
Mashujaa mjini Dodoma jana. Kampeni hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na
Hospitali ya CCBRT na Vodacom Foundation ilifanyika katika mikoa mitatu
ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa Umma na kuwasisitiza wanaume
kuwaruhusu wakinamama kujitokeza ili wakatibiwe maradhi hayo kwani
yanatibika. Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000 kwa mwaka hupatwa
na maradhi hayo wanapojifungua.
No comments:
Post a Comment