Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanikiwa kumiliki teknolojia ya kisasa
kabisa ya kusafisha maji ya chumvi na kuyafanya yawe matamu ya kunywa.
Kwa
msingi huo, Iran sasa imevunja ukiritimba wa teknolojia hiyo iliyokuwa
ikihodhiwa na Marekani, Ujerumani, Japan na Korea Kusini.
Kwa mujibu
wa Shirika Rasmi la Habari la Iran, IRNA, teknolojia hii imezinduliwa na
Taasisi ya Petrokemikali, Utafiti na Teknolojia ya Iran. Katika hafla
iliyofanyika Jumamosi alasiri, taasisi hiyo imezindua teknolojia hiyo
nadra inayotumia mbinu ijulikanayo kama Osmosis Membrane kwa kipimo cha
4040. Imedokezwa kuwa mzunguko wote wa teknolojia hiyo ni wa hapa nchini
na kwamba chombo hicho kwa sasa kina uwezo wa kuzalisha takribani lita
9,000 za maji matamu kwa siku.
Aidha chombo hicho kina uwezo kwa
kubadilisha maji ya chumvi baharini na aina mbali mbali za maji machafu
kuwa maji safi na matamu kwa ajili ya matumizi ya kila siku ya
mwanadamu. Kwa kuzingatia hitajio kubwa la maji masafi katika maeneo
mbali mbali duniani, kumiliki uwezo wa teknolojia hiyo ni hatua muhimu
sana kwa Iran kwa matazamo wa kiuchumi na kistratijia. Bei ya chombo
hicho kilichotengenezwa Iran ni nafuu zaidi kwa asilima 50
ikilinganishwa na aina sawa na hiyo inayozalishwa na nchi za kigeni.
No comments:
Post a Comment