Makamu wa
Rais wa Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) Kamran Khan ( wa pili
kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano kati ya Waziri Mkuu wa
Tanzania Mizengo Pinda (katikati) na wawakilishi wa makampuni 10 ya
Kimarekani, walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam hivi
karibuni. Bw. Khan aliongoza ziara ya wawakilishi hao wa makampuni ya
kimarekani, Wizara ya Biashara ya Marekani na MCC ili kuangalia fursa za
uwekezaji katika sekta ya nishati nchini Tanzania.
Shirika
la Changamoto za Milenia (MCC), Wizara ya Biashara ya Marekani na
makampuni 10 ya Kimarekani hivi leo wamemaliza kwa mafanikio mkubwa
ziara yao ya kuangalia fursa za biashara na uwekezaji katika sekta ya
nishati katika nchi za Tanzania.
Ziara hii
ya kwanza na ya aina yake katika historia ya miaka 11 ya MCC, ililenga
kukuza mauzo ya nje ya bidhaa zinazozalishwa na makampuni ya Kimarekani
na kuongeza uwepo wa makampuni hayo barani Afrika kwa kutambulisha kwayo
fursa mbalimbali zilizopo za uwekezaji katika sekta ya nishati. Aidha,
ziara hii ililenga kuchangia katika kufikia malengo ya Mpango Maalumu wa
Serikali ya Marekani wa Kusaidia Maendeleo ya Sekta ya Nishati barani
Afrika uitwao “Power Africa” unaolenga kuongeza mara mbili kiwango cha
upatikanaji wa umeme katika nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la
Sahara.
Makampuni
haya yalipata fursa ya kukutana na viongozi waandamizi wa Serikali ya
Tanzania ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, pamoja na
wawakilishi wa sekta binafsi ya Tanzania na asasi zisizo za kiserikali
Aidha,
wajumbe wa ziara hii walikutana na Balozi wa Marekani nchini Tanzania
Mark Childress na Naibu Waziri wa Nishati wa Marekani Christopher A
Smith. Aidha wajumbe walipata maelezo kuhusu fursa za uwekezaji katika
sekta ya nishati nchini Tanzania kutoka kwa wawakilishi wa MCC, Wizara
ya Biashara ya marekani, Shirika la Marekani la Ushirikiano wa Kimataifa
(USAID) na Chama cha Wafanyabiashara wa Kimarekani nchini Tanzania.
“Sekta ya
nishati ya Tanzania ipo tayari kwa wawekezaji wan je, tungependa
makampuni ya Kimarekani yajionee yenyewe na kusikia kutoka kwa viongozi
waandamizi wa nchi hii kuhusu fursa zilizomo nchini humu,” alisema
Kamran Khan, Makamu wa Rais wa Idara ya Usimamizi.
No comments:
Post a Comment