Akizungumza na waandishi wa habari katika Kiwanja cha Kingugia, Dk. Ndungulile amesema ameamua kuitikia Wito wa akin amama hao baada ya kuona wamedhubutu kuweka umoja wao na kuamua kujikopesha wao kwa wao ili kujikomboa na umasikini kwa kufanya shughuli zao binafsi zinazowapatia kipato.
"Mwanamke anapoamua kujishughulisha katika nyumba, thamani yake inaongezeka na kupata heshima sawa kama anayopata baba." Alisema Dk. Ndungulile
Kwa upande wake, Mlezi wa Amani Group, Fatuma Shija pamoja na Mwenyekiti wa kikundi hicho, Amina Pongwe wamempongeza sana mbunge wao kwa kuitikia wito na kuja katika uzinduzi huo.
(Picha / Habarii: Deogratius Mongela / GPL)
No comments:
Post a Comment