Okwi amefikia hatua ya kusema hivyo baada ya kutapakaa habari kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii juzi kwamba amerudi Yanga. Mchezaji huyo kwa sasa yupo kwao Uganda kwa mapumziko baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu na kuisaidia Simba kumaliza nafasi ya tatu.
Hata hivyo tetesi hizo zilikanushwa na viongozi wa Simba na wa Yanga pia wakisema hawana mpango wa kumsajili mchezaji huyo. “Hizo taarifa za Yanga kumsajili Okwi hazina ukweli wowote,” alisema ofisa habari wa Yanga Jerry Muro.
“Hayo mambo ya porojo bwana, Okwi ni mchezaji wetu halali hawezi kwenda Yanga, yupo Uganda kwenye mapumziko,” alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba Zakaria Hanspope.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana Okwi alisema: “Mimi nina akili zangu timamu, siwezi kurudi Yanga kule nilishamalizana nao na sasa mimi ni mchezaji halali wa Simba, nina mkataba nao na ninauheshimu,” alisema. Aidha mchezaji huyo alisema hafikirii kuondoka Simba kwani amejiona ni mwenye bahati na klabu hiyo.
Akizungumzia mwenendo wa Simba msimu uliopita Okwi alisema kilichotokea kwa timu hiyo kumaliza nafasi ya tatu ni suala la soka na ana imani itafanya vizuri msimu ujao.
“Nafasi ya tatu sio mbaya, lakini hiyo ndio soka, kutokuchukua ubingwa ni mambo ya soka, timu yangu inafanya usajili kwa sasa naamini ni usajili mzuri utakaotufanya tufanye vizuri msimu ujao,” alisema Okwi. Okwi alisajiliwa tena na Simba Agosti mwaka jana akitokea Yanga aliyojiunga nayo akitokea SC Villa ya Uganda.
Villa ilimtumia Okwi na Fifa baada ya mchezaji huyo kuingia kwenye na Etoile du Sahel ya Tunisia aliyojiunga nayo badaa ya kuuzwa na Simba, alijiunga na Etoile kwa dola za Marekani 300,000 mwanzoni mwa mwaka 2014 kabla ya kurudi Uganda baada ya kukorofishana na klabu hiyo ya Tunisia na ndipo alipojiunga Villa kwa mkopo kabla ya kusajiliwa na Yanga na baadaye kurudi Simba.
No comments:
Post a Comment