KLABU ya soka ya Yanga imefanikiwa kumuuza kwa mkataba wa miaka
mitatu mshambuliaji wake raia wa Liberia, Kpah Sherman aliyejiunga na
timu ya Mpumalanga Black Aces iliyopanda kucheza Ligi Kuu ya Afrika
Kusini ya PSL msimu huu.
Sherman alilazimika kuondoka nchini wiki iliyopita na kuiacha timu
yake Yanga ikiwa kwenye michuano ya Kombe la Kagame kwa ajili ya
kukamilisha vipimo vya afya na makubaliano ya kimaslahi kabla ya kusaini
kuichezea timu hiyo.
Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina gazetini kwa kuwa sio
msemaji wa timu, mmoja wa viongozi wa nafasi za juu kwenye klabu hiyo
alisema wamemuuza Sherman kwa dola 150,000 sawa na zaidi ya Sh milioni
300, ambapo klabu hiyo inatarajia kutuma fedha hizo wakati wowote baada
ya kukamilika kwa taratibu za uhamisho wake.
“Ni kweli Sherman amefuzu vipimo vya afya na kusajiliwa kwa mkataba
wa miaka mitatu na klabu ya Mpumalanga Black Aces, kila kitu kinakwenda
vizuri na sasa tunamalizia taratibu za uhamisho wake ili wenzetu waweze
kututumia malipo yetu tuweze kuyatumia kwa kuziba pengo la Sherman
katika siku mbili zilizobaki kwenye usajili wetu,” alisema kiongozi
huyo.
Kiongozi huyo alisema kuondoka kwa Sherman ni pengo kubwa kwa timu
yao kwa sababu ndiyo kwanza alianza kuzoea Ligi ya Tanzania baada ya
kuanza vibaya msimu wake wa kwanza lakini anaamini atafanikiwa huko
anakokwenda na wao wapambana kuhakikisha wanamtafuta mtu sahihi wa
kuziba nafasi yake.
“Alikuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Yanga lakini siku zote
mpira haupo kwa ajili ya burudani na biashara, pia ndiyo maana
tumemruhusu kuondoka na sisi tumepata pesa ambazo tutazitumia
kuhakikisha tunaimarisha kikosi chetu katika sehemu ambazo tumeona
zinamapungufu,” alisema kiongozi huyo.
Sherman alitua Yanga kwenye dirisha dogo la usajili msimu uliopita na
kuonesha kiwango cha juu kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe, lakini baada
ya hapo alionekana kushuka kiwango na kupoteza nafasi kwenye kikosi cha
kwanza licha kumaliza msimu akifunga mabao sita kwenye ligi katika
mechi 16 alizocheza mzunguko wa pili huku akijivunia ubingwa wa ligi ya
Tanzania Bara msimu uliopita.
kuwa Musonye alikuwa akiipendelea timu hiyo licha ya kugoma kuingia
katika vyumba vya kubadilishia nguo, ambapo tayari timu hiyo ilishaonywa
huko nyuma kwa kitendo kama hicho. Timu hiyo juzi iligoma tena kuingia
katika vyumba vya kubadilishia nguo wakati wa mchezo wa fainali ya
Kagame dhidi ya Azam FC, ambao walifungwa 2-0 na kushindwa kutwaa taji
hilo.
Wakizungumza na waandishi kwa nyakati tofauti kuhusu ugomvi wao,
viongozi wote wawili walikiri kushikana mashati, huku Musonye akisema
lazima wawekeane heshima. Musonye hakusema sababu ya wao kushindwa
kuelewana akijitetea kuwa katika masuala ya soka, kusuguana ni jambo la
kawaida, hivyo walikuwa wakiwekeana heshima. “Tumeshayamaliza ilikuwa ni
jambo dogo tunawekeana heshima. Kwenye soka mambo ndivyo
yalivyo,”alisema.
Mgoi aliweka bayana kuwa Musonye alikuwa akitaka mgeni rasmi wa
mashindano hayo awe Odinga ambaye alikuwa uwanjani hapo kushuhudia
fainali za Gor Mahia na Azam. Alisema TFF haikuwa na taarifa kutoka
serikalini kuwa Odinga atakuwa nchini kwa ajili hiyo, hivyo tayari
walimuandaa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki kuwa mgeni
rasmi.
Alisema baada ya TFF kuweka msimamo wao kama waandaaji wa mashindano
kwa mgeni wao ambaye ni Sadiki, Musonye alianza kutoa maneno makali na
kuanzisha vurugu. Hatahivyo, kama ilivyopangwa na TFF, Mkuu huyo wa mkoa
wa Dar es Salaam ndiye aliyetoa zawadi kwa Azam ambao ni mabingwa wapya
wa Afrika Mashariki na Kati.
Pamoja na hilo, Mgoi alisema Musonye alikuwa akionesha upendeleo
dhidi ya timu hiyo ya Kenya akiitetea timu ya Gor Mahia ambayo ilikiuka
onyo ililopewa awali la kutoingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo
kwa imani za kishirikina.
Alisema timu hiyo ilivunja kitasa katika sehemu ambazo walikatazwa
awali kuingia, na wao kutumia nguvu na kufanya lolote kwa vile tu
walikuwa wakitetewa na katibu huyo wa Cecafa.
“Gor Mahia imekuwa na dosari nyingi ikiamini haiwezi kufanywa lolote
na tunapomshirikisha Musonye hakutoa ushirikiano na badala yake amekuwa
mtu wa kuitetea, ndio maana alipoonesha upendeleo wake, nasi tulisimama
kuonesha uzalendo wetu,”alisema na kuongeza kuwa, timu hiyo imekuwa
ikifanya uharibifu ikisaidiwa na kituo kilichokuwa kinarusha matangazo
ya soka cha Supersport.
Kitendo hicho cha Gor Mahia kutoingia katika vyumba vya kubadilisha
nguo sio cha kwanza, kwani katika mchezo dhidi ya Yanga walipita katika
sehemu ambapo hupaki magari ya kurusha matangazo ya soka kwenye
televisheni na kupewa onyo la kutorudia.
No comments:
Post a Comment