Hofu ya kushambuliwa waandishi yatanda Nigeria
Wanaharakati wa vyombo vya habari nchini Nigeria wameingiwa na wasiwasi
kutokana na kuongezeka mashambulio ya vyombo vya usalama vya serikali
dhidi ya waandishi wa habari. Jumuiya na asasi za kutetea waandishi wa
habari zimeingiwa na wasiwasi huo baada ya waandishi wanne wa habari
kushambuliwa ndani ya kipindi cha wiki moja. Muhammad Atta-Kaffin-Dangi,
ni mmoja wa waandishi hao wa habari ambaye alishambuliwa na polisi
katika mji wa Gwagwalada kwa kisingizio cha kuandaa ripoti bila ya kuwa
na kibali. Victor Akinkuolie, ni mwandishi mwengine wa habari ambaye
naye pia ameshambuliwa na vikosi vya usalama ambapo kabla yake
alishakabiliwa na vitisho mara kadhaa. Joseph Hir na Kamarudenn
Ogundele ni waandishi wengine wawili wa habari walioshambuliwa katika
kipindi cha juma hili katika maeneo tofauti ya Nigeria na wafuasi na
watu wa karibu wa viongozi wa majimbo. Vitendo vya utumiaji nguvu dhidi
ya waandishi wa habari vimeitia wasiwasi kamati ya kulinda waandishi wa
habari yenye makao yake mjini New York, Marekani. Kamati hiyo imemtaka
rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari aanzishe uchunguzi kuhusiana na
kushambuliwa waandishi wanne hao wa habari pamoja na kuchukua hatua za
kuhakikisha uhuru wa magazeti na vyombo vya habari nchini humo unalindwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment