Rwasa: Uchaguzi Burundi uwe umeshafanyika Agosti
Kiongozi wa upinzani nchini Burundi Agathon Rwasa amesema uchaguzi wa
rais lazima uwe umefanyika ifikapo mwezi Agosti, hata hivyo amesisitiza
kwamba uchaguzi hauwezi kuwa huru na wa haki pasina kuwepo usalama na
vyombo huru vya habari. Uwezekano wa uchaguzi wa rais kufanyika tarehe
26 mwezi huu wa Juni unaonekana kuwa mdogo kutokana na kuendelea
maandamano kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa ya kupinga uamuzi wa Rais
Pierre Nkurunziza wa kuamua kugombea urais kwa muhula wa tatu. Tayari
uchaguzi wa bunge na wa serikali za mitaa umeakhirishwa kutokana na
machafuko ambayo hadi sasa yamesha sababisha vifo vya watu zaidi ya 30.
Rwasa, ambaye naye pia ni mgombea katika uchaguzi wa rais amesema ni
lazima uchaguzi wa rais uwe umefanyika ifikapo tarehe 26 ya mwezi Agosti
wakati kipindi cha sasa cha urais kitakapomalizika. Rwasa amesisitiza
kuwa hakuna nafasi kwa ajili ya serikali ya mpito. "Ni wajibu kwa wote
kuheshimu katiba kwa kuzingatia kwamba ilikuwa ikifahamika tokea kabla
kuwa hadi ifikapo tarehe hiyo rais na wabunge wapya wanapaswa wawe
wamechaguliwa", amesema. Tume ya uchaguzi ya Burundi CENI ilitangaza
siku ya Jumatano iliyopita uamuzi wa kuakhirisha chaguzi za bunge na
serikali za mitaa pasina kueleza chochote kuhusu uchaguzi wa rais
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment