Stamili Mponzi mkazi wa kijiji cha Ikule wilayani Kilombero, mkoani Morogoro anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumchoma mwanae na kumjeruhi mikono kwa madai ya kuiba ugali.
Mama huyo alimuunguza mwanaye Joseph Chawala, akimtuhumu Kuiba Ugali, kwa mujibu wa watendaji mbalimbali wa kata ya Mng’eta.
Wakizungumzia
tukio hilo Jerome Chulu na Jeneth Hetela, walisema unyanyasaji huo
ulishuhudiwa na majirani wa mwanamke huyo baada ya kusikia kelele za
watoto ambao walimchukua mtoto huyo kumpeleka ofisi ya mtendaji wa
kata,polisi na baadaye hospitali.
Walibainisha
baadaye kuwa polisi walikwenda kumkamata mwanamke huyo na mumewe
Halidi Kiwenji ambaye inadaiwa alikuwa karibu wakati wa tukio hilo
ingawa baadaye baba huyo aliachiwa ili akawaangalie watoto wengine
nyumbani.
Polisi walithibitisha tukio hilo ambalo uchuguzi wake unaendelea ili kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo.
Wananchi mbalimbali waliohojiwa wametaka hatua kuchukuliwà kwa watu wanaoendekeza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
Wananchi mbalimbali waliohojiwa wametaka hatua kuchukuliwà kwa watu wanaoendekeza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment