|
|
Uchaguzi wa 25 wa bunge la Uturuki umeanza leo nchini humo. Vituo vya
kupigia kura vilifunguliwa saa mbili asubuhi kwa saa za Uturuki ambapo
wananchi zaidi 53,741,000 waliotimiza masharti ya kupiga kura
wanawachagua wabunge 550 wa bunge la nchi hiyo. Kwa mara ya kwanza
katika uchaguzi huo chama kinachounga mkono Wakurdi kitwacho Chama cha
Demokrasia ya Wananchi (HDP) kinashiriki katika sura ya chama cha siasa,
na endapo kitakafanikiwa kupata asilimia 10 ya kura inayotakiwa kuweza
kuingia bungeni, kitaweza kupunguza viti 50 hadi 60 kati ya viti vyote
vinavyoshikiliwa na chama tawala cha Uadilifu na Maendeleo (AKP). Askari
wapatao laki nne wamesambazwa katika maeneo mbalimbali ya Uturuki ili
kulinda usalama wakati wa zoezi la uchaguzi. Waturuki waishio nje ya
nchi walipiga kura zao kuanzia tarehe 8 hadi 31 ya mwezi uliopita wa
Mei. Chama tawala cha AKP ambacho kinashikilia hatamu za uongozi kwa
zaidi ya muongo mmoja sasa kinapigania kunyakua theluthi mbili ya viti
vya bunge ili kuweza kuubadilisha mfumo wa utawala wa bunge kwa
kuanzisha mfumo wa urais. Vyama vitatu vikubwa zaidi vya upinzani nchini
Uturuki, vyote vimetangaza kuwa vinapinga mfumo wa utawala wa urais
No comments:
Post a Comment