Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema matamshi
ya hivi karibuni yaliyotolewa na viongozi wa Marekani kuhusu mazungumzo
ya nyuklia ya Iran ni ya kipropaganda. Ali Larijani ameyaeleza hayo
katika mahojiano na gazeti la Kiarabu la Al Wifaq na kuongeza kuwa
misimamo iliyoonyeshwa hivi karibuni na viongozi wa Marekani kuhusiana
na mazungumzo ya nyuklia kati ya Iran na nchi zinazounda kundi la 5+1 ni
ya kipropaganda na yenye lengo la kutatua matatizo ya ndani ya nchi
hiyo na kuzuia hujuma za lobi zenye misimamo mikali za Wazayuni. Dakta
Larijani amesema propaganda za Marekani zitakuwa na taathira hasi katika
mazungumzo ya nyuklia, lakini kwa kuwa na uelewa kamili wa propaganda
hizo, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeifanya mantiki kuwa ndio msingi wa
harakati yake katika mazungumzo hayo. Kuhusiana na matukio ya Yemen na
kuzuiliwa kufikishwa nchini humo misaada ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran,
Spika wa Bunge amesema mzingiro dhidi ya wananchi wa Yemen hautokuwa na
tija nyengine ghairi ya kuharibu jina la Saudi Arabia katika historia.
Ameongeza kuwa shambulio la Saudia nchini Yemen limetokana na kosa la
utawala wa Aal Saudi katika kutathmini masuala ya Mashariki ya Kati, kwa
sababu haiwezekani kuwaburuza wananchi wa mataifa ya eneo hili
No comments:
Post a Comment