Rais Omar al-Bashir wa Sudan ameunda serikali mpya, mwezi mmoja
tangu alipopata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa rais uliosusiwa na
upinzani na kutawaliwa na madai ya kufanyika udanganyifu. Al Bashir
alitangaza baraza lake jipya la mawaziri hapo jana ambapo amemteua
msaidizi wake Ibrahim Ghandour kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Mohamed
Zayed kuwa Waziri wa Mafuta. Rais wa Sudan mwenye umri wa 71 amemwondoa
pia waziri wake wa ulinzi wa muda mrefu Abdulrahim Mohamed Hussein na
kumteua Mkuu wa majeshi Luteni Jenerali Mustafa Othman Obeid kuwa waziri
mpya wa ulinzi. Al Bashir aidha amewabakisha katika yadhifa zao makamu
wake wawili Bakri Hassan Saleh na Hassabo Mohamed Abdelrahman. Kwa
mujibu wa shirika la habari la serikali la al-Sudan serikali mpya ya Al
Bashir itakuwa na jumla ya mawaziri 31. Aidha mapema leo Rais wa Sudan
ametoa dikrii ya kuteua magavana wa majimbo 18 ya nchi hiyo ambapo
waziri wa zamani wa ulinzi Abdulrahim Mohamed Hussein ameteuliwa kuwa
gavana wa jimbo la Khartoum. Al-Bashir alichaguliwa tena kuwa rais wa
Sudan katika uchaguzi uliofanyika mwezi Aprili baada ya kujipatia
asilimia 94 ya kura. Wakati alipokula kiapo cha urais, Rais wa Sudan
aliahidi kufungua ukurasa mpya kwa ajili ya nchi hiyo na kurejesha
uhusiano na madola ya Magharibi pamoja na kupambana na ufisadi. Omar
Hassan Al Bashir, aliingia madarakani mwaka 1989 kupitia mapinduzi ya
kijeshi
No comments:
Post a Comment