Shirika la Afya Duniani, WHO nchini
Tanzania limesema idadi ya maambukizi mapya ya ugonjwa wa Kipindupindu
miongoni mwa wakimbizi wa Burundi waliokimbilia mkoani Kigoma nchini
Tanzania imepungua baada ya visa zaidi ya 4,400 kuripotiwa na wagonjwa
30 kufariki dunia. WHO imesema visa vipya vya kipindupindu kwa siku
vimepungua kutoka 915 tarehe 18 mwezi huu hadi 100 kwa sasa na hali hiyo
imesababishwa na hatua zilizochukuliwa kudhibiti mlipuko ikiwemo
kuimarisha huduma za maji safi.
WHO inasema harakati za kudhibiti
Kipindupindu zinafanywa kwa ushirikiano baina ya serikali ya Tanzania na
wadau kama vile Umoja wa Mataifa na madaktari wasio na mipaka, MSF.
Dokta Rufaro Chatora, mwakilishi wa WHO nchini Tanzania amesema licha
ya visa vya kipindupindu kushuka katika siku chache zilizopita, hali
bado ni mbaya mno. Ameongeza kuwa mbali na kipindupindu WHO pia
tunasimamia shughuli zingine za kiafya mathalani kwa siku kuna wazazi 72
wanajifungua. Wakati huo huo shirika la kuhudumia
wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema idadi ya wakimbizi wa
Burundi wanaoingia Tanzania imepungua. Takribani watu laki moja
wamekimbilia nchi jirani kutoka Burundi baada ya ghasia kuanza nchini
humo mwezi Aprili kufuatia tangazo la Rais Pierre Nkurunziza kuwa
atawania urais kwa muhula wa tatu. Maandamano bado yanaendelea Burundi
kupinga uamuzi huo
Mwenyekiti wa Chama cha
Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar Bi. Maryam Hamdani akifungua
mafunzo ya siku mbili ya waandishi wa habari kuhusu Haki za binaadamu na
sheria za waandishi wa Habari katika kituo cha Huduma za Sheria
Zanzibar kiliopo Migombani.
Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ
Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ
No comments:
Post a Comment