wadau wakiwa tayari kwa uzinduzi
Lowassa awekwa mtu kati Monduli
WAKATI wakongwe wa siasa wakimhadharisha aliyekuwa Waziri Mkuu,
Edward Lowassa, kutofuata mashabiki wanaomtaka ahame CCM ambako
amelelewa na ndiko anakoheshimika, madiwani 20 wa chama hicho katika
Jimbo la Monduli, wamejiunga na Chadema.
Madiwani hao wameingia Chadema na kufuatwa na wenyeviti sita wa vijiji pamoja na viongozi wa jumuiya za CCM, huku wakimwomba Lowassa ambaye ni Mbunge wa jimbo hilo, kufanya kinachoitwa ni uamuzi mgumu wa kuwafuata, baada ya CCM kukata jina lake sambamba na wagombea urais wengine 33, wakiwemo waliowahi kuwa mawaziri wakuu kama yeye.
Akizungumza jana katika mkutano wa hadhara, kabla ya kukabidhi kadi yake na za wenzake 19 wa CCM kwa viongozi wa Chadema, kiongozi wa Madiwani hao, Julius Kalanga kutoka Kata ya Lepurko, alisema wamefanya uamuzi aliouita mgumu, ambao Lowassa amekuwa akiuzungumza.
“Sisi tumeamua kujiunga Chadema kutafuta haki na kuondoka CCM ambako wanachakachua Katiba ya Chama kwa kumpitisha kiongozi wanayemtaka, badala ya kufuata Katiba na wananchi wanachotaka. “Tunamwomba Mheshimiwa wetu Lowassa, atufuate huku Chadema, afanye uamuzi mgumu aliokuwa akisema kila siku na asiogope kuhama… atakuwa amefanya uamuzi wenye tija kwa Taifa,” alisema Kalanga.
Diwani huyo pia aliwasihi wananchi kufuata madiwani wao wanakokwenda kwa sababu hata huko watachukua fomu na kugombea ili kuing’oa CCM madarakani.
Waliohama
Madiwani waliohama chama ni wa kata ya Engaruka, Engutoto, Esilalei, Loksale, Majengo, Makuyuni, Meserani, Nalalani, Lemooti, Moita, Monduli Juu, Monduli Mjini, Mferejini, Mswakini, Mto wa Mbu, Migungani, Selela, Sepeko na Lashaini.
Madiwani na viongozi hao ni Kalanga mwenyewe, Edward Lenanu, Bazir Siamini, Sigur Olekibinti, Loti Yamat, Goodluck Lerunya, Pashet Sengurumi, Yase Runja, Gidion Kimongishu, Dora Kipuyo, Mary Morindat, Sara Lomayan na Halima Lusinde.
Wengine ni Dotto Mlacha, Hawa Nyambiry, Alex Kamanda, Sion Kapela, Maria Lemta, Onesmo Naikoyo, Shaban Adam, Enditosidai Naikulo na Elifuraha Simon.
Pia yupo Dinna Solomon, Loti Naparana, Jocy Laizer, Edward Mathayo, Piniel Loning’o, Napir Mukare, Inot Leringa, Kalaine Lowassa, Maria Mepukori, Mary Stivin na Edward Kone.
Ushauri wa wakongwe
Mwito huo wa madiwani wa Monduli, unatofautiana na ushauri wa kada mkongwe wa CCM, Steven Mashishanga, aliyekaririwa akimtaka Lowassa atulie na aachane na ushawishi wa watu wanaomtaka ahame chama hicho.
Mashishanga katika mahojiano yake na gazeti moja la kila siku juzi, alimkumbusha Lowassa kuwa bado ni kiongozi anayeheshimiwa na jamii na kumuasa kuwa kama anahisi ameonewa, asamehe.
Akifafanua hoja zake, Mashishanga alisema wanaomshawishi Lowassa ahame CCM na wale wanaohama chama hicho kwa sababu ya kukatwa kwa jina la Lowassa katika kuwania urais, si wana CCM wa uhakika.
Kwa mujibu wa Mashishanga, ndani ya CCM mgombea akiteuliwa, wanachama huachana na yaliyopita na kuwa wamoja kwa ajili ya kukiendeleza chama.
Malaigwanani
Mbali na Mashishanga, pia wazee wa kimila wa jamii ya wafugaji wa Kimasai, maarufu malaigwanani kutoka Wilaya ya Monduli, nao wamemuomba Lowassa kuendelea kuwa kada wa CCM, kwa sababu ndicho chama kilichomlea na anakijua.
Mmoja wa malaigwanani, Mzee Joseph Mesopiro, kutoka Kata ya Sepeko, alikaririwa na vyombo vya habari kwa niaba ya malaigwanani akisema, wanakusudia kutuma ujumbe maalumu kwa Lowassa, utakaomshauri asihame CCM kama baadhi ya watu aliowaita wapambe wanavyomshauri.
Laigwanani mwingine, Julius Laizer kutoka Kata ya Moita, alisema bado anaamini kuwa CCM itaendelea kubaki imara, hata kama baadhi ya watu watakihama.
Lazier alisema viongozi waliolelewa na kukuzwa CCM, wanaamini chama hicho kitaendelea kuwa imara na hawako tayari kukubali ushawishi wowote wa kutaka wahamie upinzani.
Naye Mwenyekiti wa CCM Kata ya Lepurko wilayani Monduli, Njoput Alami, alikaririwa akibeza taarifa za kushawishi watu kuhama CCM kwa kisingizio cha Lowassa kukatwa katika majina ya wawania urais, akiziita ni kelele za wapambe wanaohofia kukosa fursa walizotarajia, iwapo Lowassa angeteuliwa kuwa mgombea urais wa CCM.
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa aliwakaribisha na kusema Chadema watu wote wanapendana na hakuna ukubwa wala uongozi, hivyo wanapokuja huko ni kazi moja ya ukamanda kuwatumikia wananchi.

Benki kuu Tanzania imejibu kwanini sarafu mpya ya shilingi 500 haipo sana kwenye mzunguko
Kwenye hii post tumeipata benki kuu ya Tanzania ambayo iko tayari
kuzungumzia ishu ya sarafu mpya ya shilingi mia tano kutoonekana sana
kwenye mzunguko wa fedha nchini Tanzania.
‘Benki kuu iliamua kubadilisha kutoka noti na kuleta sarafu ya shilingi mia tano baada ya kuona noti hiyo inakuwemo kwenye mzunguko kwa muda mrefu kuliko inavyotakiwa bila kurudishwa Benki hivyo inachakaa mno’

‘Katika zoezi hilo la kuibadilisha
noti ya shilingi mia tano kuwa sarafu, utakuta kwamba Benki kuu sehemu
sehemu ambayo inaanza usambazaji ni kwamba wanatoa pesa kwa benki za
biashara na zinapokuja huwa tunawatolea wachukue sarafu na noti lakini
kwenye kipindi hiki benki hizi zimekua hazichukui sana sarafu ya
shilingi mia tano kama zinavyochukua noti, ila sarafu hii ipo kabisa‘
Matokeo ya Azam vs KCCA ya Uganda yasikupite mtu wangu!!
Klabu ya Azam imeanza vyema michuano ya kombe la Kagame inayoendelea kwenye uwanja wa Taifa, Dar es salaam baada ya kuwafunga KCCA ya Uganda bao 1-0.
John Boko ndiye aliyeiwezesha timu yake kuibuka na ushindi katika kipindi cha kwanza dakika ya 12 akipokea pasi kutoka kwa Shomari Kapombe.
Yanga ilianza vibaya michuano hiyo jana baada ya kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.
WAKAZI WA JIJI LA MWANZA WAJITOKEZA KUMLAKI KWA SHANGWE DKT MAGUFULI JIJINI MWANZA LEO
Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia Wananchi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kwa wingi jioni ya leo.
Mgombea
Uraisi kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Mh.Dkt John Pombe
Magufuli akiwasalimia wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi wa
jiji la Mwanza na vitongoji vyake,nje ya ofisi za CCM mkoa,ambao
walijotokeza kumlaki kwa shange na furaha kubwa.Dkt Magufuli amewasili
leo jijini Mwanza akitokea jijini Dar kwa ajili ya kujitambulisha kwa
wanachama wa chama hicho
Full Time:Yanga wapigwa 2-1 ,Canavaro akosa Penati
Klabu ya Yanga imeshindwa kuonyesha makali yake baada ya kukubali
kipigo cha Magoli mawili kwa moja kutoka kwa klabu ya Gor mahia ya Nchni
kenya.
Katika mcehzo huo Yanga ilikua ya kwanza kupata goli kupitia mshambuliaji wake Donald Ngoma katika dakika 4 ya kipindi cha kwanza.
Hali ya mchezo ilibadilika na Gor mahia walicheza kwa kasi kuhakikisha wanasawazisha goli hilo na juhudi zao zilizaa Matunda baada ya Mshambuliaji wao Harun Shakava kutingisha nyavu za Yanga katika Dakika ya 18 kipindi cha kwanza.
Dakika ya 23 Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma alitolewa kwa Kadi nyekundu na mwamuzi wa mchezo huo Ssali Mashood baada ya kumfanyia madhambi Harun Shakava wa Gor Mahia.
Mpaka mapumziko timu hizo zilienda sare ya goli moja kwa moja ambapo katika kipindi cha pili dakijka ya 61 Michaeli olunga aliipatia Gor Mahia goli la pili,
Dakika ya 72 ya mchezo huo Nadir Haroub Canavaro alikosa penalti

CHADEMA wamejipanga hivi kwenye kuchukua fomu za kugombea Ubunge na Udiwani 2015
Kuanzia July 15 hadi 19 mwaka huu
2015 CHADEMA wameanza rasmi utaratibu Wagombea wa Ubunge na Udiwani
kuchukua na kurudisha fomu kwenye Majimbo yenye Wabunge wa chama hicho.
Baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
kutangaza majimbo mapya 26 ya Uchaguzi, CHADEMA imelazimika pia
kupangua ratiba ya awali na sasa kimeruhusu wanachama wote wenye sifa
kuchukua na kurudisha fomu za kuwania uteuzi wa ndani ya chama katika
nafasi za udiwani na Ubunge katika majimbo yote ya Uchaguzi nchi nzima.
Wagombea wa Udiwani wao ratiba iko
tofauti kidogo, watachukua kurudisha fomu katika kata zote Tanzania
kuanzia July 15 2015 hadi July 29 2015 saa 10 jioni.
“Wagombea
ambao walishachukua na kurejesha fomu wana haki ya kuamua jimbo lipi
wanaenda kugombea na hawalazimiki kuchukua fomu upya…watatakiwa
kuujulisha uongozi wa chama ngazi ya jimbo kwa barua rasmi kuonesha kuwa
fomu yake iwe ni ya jimbo lipi kati ya jimbo mama ama jipya na nakala
ya barua hiyo inakiliwe ngazi ya wilaya, mkoa, kanda na taifa,
CUF ‘washikilia’ urais wa Ukawa
KITENDAWILI cha Chama cha Wananchi (CUF) kuridhia hoja ya Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa) kusimamisha mgombea mmoja wa nafasi ya urais
kwa upande wa vyama vya upinzani, kinatarajiwa kuteguliwa Jumamosi ya
wiki ijayo, ambapo Baraza Kuu la Uongozi wa Taifa wa chama hicho litakaa
kujadili na kutoa uamuzi.
Hii ina maana kwamba, kama Baraza Kuu likipinga, itakuwa rasmi kwamba ndoto za vyama vya upinzani kusimamisha mgombea mmoja zitafutika.
Hayo yalibainishwa jana Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu Bara wa CUF, Magdalena Sakaya alipokuwa akizungumzia ushiriki wao kwenye Ukawa pamoja na kutohudhuria kwao juzi kwenye kikao cha Ukawa kujadili majimbo ya uchaguzi na kumtaja mgombea nafasi ya urais kupitia kundi hilo.
Sakaya alisema CUF ni sehemu ya Ukawa na wanaendelea kushiriki kwenye vikao vya kuafikiana maamuzi kwa hoja mbalimbali na kwamba hawajajitoa kwenye Ukawa kama ambavyo baadhi ya mitandao na vyombo vya habari vimeripoti. “Hatujajitoa Ukawa, sisi ni sehemu ya Ukawa na hatuwezi kusaliti kitu tulichokiasisi wenyewe,” alisema Sakaya.
Na kuongeza, taharuki iliyopo mitaani kwamba CUF wamejitoa inachangiwa na baadhi ya vyombo vya habari ambavyo siku chache zilizopita vimekuwa vikiripoti kwamba Ukawa imeshamteua mgombea nafasi ya urais, jambo ambalo limezua taharuki kwa wanachama wa CUF, kwa kuwa hawajatoa ridhaa hiyo.
Alisema kutokana na taharuki hiyo, wanachama wameingiwa na hofu ya jambo hilo kwa kuwa hakuna ridhaa iliyoafikiwa na vikao vya maamuzi, na kwamba hali hiyo imeifanya chama hicho kuitisha kikao cha Baraza Kuu la Uongozi, chombo ambacho ndicho chenye maamuzi ya kutoa ridhaa hiyo.
“Baada ya kuona habari hizo kwenye baadhi ya vyombo vya habari na mitandaoni, wanachama wetu wameingiwa na hofu ya ushirikishwaji na tumeitisha Baraza Kuu la Uongozi litakutana Julai 25, mwaka huu, tutajalidi na kutoa uamuzi wetu,” alisema Sakaya.
Kuhusu kushirikishwa kwao ndani ya Ukawa, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Abdul Kambaya alisema kwa mfano kikao cha juzi kilichofanyikia hoteli ya Colosseum, Dar es Salaam, walipata taarifa baada ya kikao kuanza, hivyo walishindwa kuhudhuria kwa kuwa walikuwa kwenye kikao cha dharura cha wanachama wao.
“Hizo taarifa za kikao cha Ukawa cha kumtangaza mgombea na kuzungumzia majimbo ya uchaguzi mapya, mwenyekiti wetu alipata taarifa mara baada ya kikao kuanza majira ya saa nne asubuhi, baada ya kuonekana hayuko, hakuweza kuhudhuria kwa kuwa tulikuwa kwenye kikao kingine cha wanachama wetu”, alisema Kambaya.
Aliongeza kuwa, kikao hicho cha jana taarifa za uwepo wake hazikuwa wazi mapema na kwamba mwakilishi wao aliyehudhuria ni wa ngazi ya wataalamu na sio ngazi ya viongozi wakuu, ambao ndio wenye maamuzi.
Kutokana na hali hiyo, alisema mkutano wa Julai 25 ndio utakaotoka na maamuzi ya ama kukubali maridhiano ya Ukawa ya kusimamisha mgombea mmoja au vinginevyo.
“Tunaomba tusubiri baraza la maamuzi likae, sisi tunafanya kazi kwa kushirikisha wanachama wetu na baraza hilo, litakuja na maamuzi ya masuala yote ya uchaguzi na mengineyo,” alisema Kambaya.
Juzi, katika kikao cha Ukawa kilichofanyika hoteli ya Colosseum kilihudhuriwa na viongozi wa juu wa vyama vinavyounda kundi hilo, isipokuwa kiongozi wa CUF, na kilipangwa kumtaja mgombea mmoja wa urais kupitia kundi hilo atakayechuana na wagombea wengine, akiwemo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli.
Hata hivyo katika kikao hicho kilichokaa hadi usiku saa tatu, hakikumtaja mgombea wa nafasi hiyo na badala yake kilisema jina la mgombea wanalo na kwamba watalitangaza ndani ya siku saba.

DAMN! TRICKY Movie:Uzinduzi wake kufana kupita kifani ndani ya Mbeya
Kama wewe ni mkazi wa jiji la Mbeya hii siku ni kubwa sana ambayo hautakiwi kukosa kwani itakuwa siku ya uzinduzi wa filamu kubwa ndani ya Mbeya.Watu wengi watakuwepo siku hiyo kwani inatazamiwa kubadili soko la filamu ndani ya Mbeya na Nyanda za juu kusini kiujumla.
Hii ndiyo Location itakayotumika kuzindulia movie kwa mara ya kwanza Outdoor pool Party Swagger,Karibu sana JM HOTEL Tarehe 25 July 2015

OUTDOOR POOL |
MHE. MAGUFULI APOKELEWA KWA KISHINDO DAR, AHUTUBIA NYOMI MBAGALA
…Magufuli akisalimiana na wanachama wa CCM. |
KIKAO CHA UKAWA KUMPATA MGOMBEA URAIS KINAENDELEA MUDA HUU
Wajumbe wa kikao hicho wakipata futari wakati wa mapumziko. |
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.
Wilbroad Slaa (kulia) na Mwanasheria wa chama hicho, Tundu
Lissu wakipata futari wakati wa mapumziko.
|
POLISI WATANGAZA ZAWADI YA MILLION 50 KWA YEYOTE ATAKAYEFANIKISHA HILI
Jeshi la polisi Tanzania
limetangaza kutoa zawadi nono ya shilingi za kitanzania million 50 kwa mtu yeyete
mwenye taarifa za uhakika na za haraka zitakazofanikisha kuwakamata wote
waliovamia kituo cha polisi stakishari na kuua askari na raia waliokuwa katika
kituo hicho usiku wa kuamkia jana.
Akitoa Taarifa mbele ya
wanahabari leo kamishna wa polisi kanda maalum ya dare s ealaam SULEMAN KOVA amesema kuwa kupitia dhana ya polisi ya ulinzi
shirikishi mkuu wa jeshi la polisi IGP ERNEST MANGU ameona ni muhimu
kuwashirikisha wananchi kikamilifu katika suala hili linalohusiana na ulinzi na
usalama wao na watanzania wote kwa ujumla. Mtu yeyote atakaye jishughulisha na hili kwa kutoa Taarifa sahihi atoe Taarifa kwa vioongozi wakuu wa jeshi la polisi waliopo karibu au apige namba zifuatazo---
KAMISHNA WA POLISI
KANDA MAALUM (CPS.H KOVA) -----0754034224
MSEMAJI WA JUESHI LA
POLISI (SSP ADVERA BULIMBA)-----0713631667
MKURUGENZI WA MAKOSA YA
JINAI (CP DIWANI ATHMAN)----0715323444
Aidha wananchi wenye
taarifa husika pia wanaweza kuonana uso kwa uso na viongozi wakuu wa makao
makuu ya polisi au kanda maalum na kuwapa taarifa moja kwa moja
Kamishna kova amesema
kuwa mwananchi ambaye ataleta taarifa husika na kufanikisha zoezi hilo
itafanyika siri kubwa na hatajulikana popote kama yeye ndiye mtoa taarifa
husika
HIVI NDIVYO KITUO CHA POLISI KILIVYOCHOMWA MOTO..
TUKIO la
wananchi kuchoma Kituo Kidogo cha Polisi cha Bunju A kilichopo wilayani
Kinondoni, jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita lilizua mshtuko wa
aina yake na kuweka rekodi mbaya nchini, Uwazi linakupa habari kamili.
Chanzo cha wananchi hao kuchoma kituo
hicho kilielezwa kuwa ni baada ya mwanafunzi wa darasa la nne katika
Shule ya Msingi Bunju B aliyetajwa kwa jina la Tabia Omary (11) kugongwa
na daladala Julai 10, mwaka huu alipokuwa anavuka kuelekea shuleni.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo
aliyejitambulisha kwa jina la Miriamu Njuki, katika eneo lililotokea
ajali, alikuwepo askari wa usalama barabarani akisaidia watoto hao
kuvuka barabara kwa kusimamisha magari lakini dereva huyo wa daladala
alikaidi na kumgonga mwanafunzi huyo na kufariki papo hapo.
“Baada ya askari huyo kuona daladala
limefanya tukio hilo na kutosimama, ilibidi ajiongeze na kuanza
kukimbizana na nalo kwa kutumia gari lingine ambapo alifanikiwa
kumkamata dereva huyo,” alisema Miriamu.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ambaye
hakutaka jina lake litajwe gazetini, alisema baada ya askari kumkimbiza
dereva huyo na kuuacha mwili wa marehemu barabarani kwa muda mrefu ndipo
wananchi hao walipopatwa na jazba na kwenda kuchoma moto kituo cha
polisi jambo ambalo halikuwa sahihi.
“Hakuna uhusiano wowote kati ya
mwanafunzi huyo kugongwa na kuchomwa kituo cha polisi kwa sababu kituo
chenyewe kipo umbali mrefu na eneo alipogongewa mwanafunzi huyo,
walikuwa na chuki zao tu,” alisema mkazi huyo.
Imeelezwa kuwa wananchi hao baada ya kuchoma moto kituo, wengi wao walikimbilia mikoani kukwepa kukamatwa.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule
Msingi Bunju B, Ezekiel Johnson, amesema kukosekana kwa matuta katika
eneo hilo kunachangia ajali nyingi kutokea.
“Mpaka sasa wameshagongwa watoto wanne
na kati yao, wawili wamepoteza maisha na wawili wamepata ulemavu wa
kudumu tangu mwaka huu uanze,” alisema mwalimu huyo.
Katika tukio hilo, wahalifu hao licha ya
kupasua vioo na kuiba spea za magari kadhaa yaliyokuwepo kituoni hapo,
walifanya uharibifu mkubwa katika gari la mwanamke aliyetambuliwa kwa
jina la Husna Shabani
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck
Sadick aliyekwenda kushuhudia tukio hilo alieleza masikitiko yake kwa
wananchi waliochukua sheria mkononi na kumuagiza Kamanda wa Polisi, Mkoa
wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura kuhakikisha watuhumiwa wote
wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Jeshi la polisi linawashikilia zaidi ya
watu 32 kwa tuhuma za kukichoma kituo hicho na upelelezi unaendelea.
Marehemu Tabia alizikwa Jumamosi iliyopita katika mtaa wa Chalinze Bunju
B ambao ndugu, jamaa na marafiki waliokuwa na simanzi waliangua vilio
kwa kuondokewa na mpendwa wao huyo.
Shein: Magufuli ndiye kiboko yao
RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amesema uteuzi wa mgombea wa
CCM katika nafasi ya rais wa Jamhuri ya Muungano katika uchaguzi mkuu,
Dk John Magufuli ndio chaguo sahihi la kupambana na upinzani na kuleta
ushindi katika CCM na kushika dola.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili Zanzibar kutoka Dodoma, Dk Shein alimtaja Magufuli kama kiongozi hodari muaminifu mwenye shauku kubwa ya kuleta maendeleo ya nchi yake.
Dk Shein katika mkutano mkuu uliomalizika Dodoma hivi karibuni Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi imemwidhinisha kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM tayari kupambana na chama kikuu cha CUF.
Alisema, Magufuli katika nyadhifa mbalimbali alizoshika ameonesha uhodari wa kuchapa kazi na uzalendo pamoja na kusimamia majukumu yake pamoja na walio chini yake. Alifahamisha kwamba ndiyo kigezo sahihi cha kupambana na wapinzani na kuleta maendeleo ya wananchi wa Tanzania.
‘’Mimi namfahamu vizuri sana Magufuli nimefanya kazi naye katika kipindi cha miaka 9 katika baraza la mawaziri nikiwa makamu wa rais......ni mchapa kazi hodari, mwadilifu mwenye mapenzi makubwa na wananchi wake,’’alisema.
Kwa mfano alisema katika Wizara zote alizopata kufanya kazi alionesha uwezo wa ubunifu wa kuleta maendeleo akizitaja Wizara ya Uvuvi pamoja na Ujenzi.
Aidha alimpongeza kwa kumteua Samia Suluhun Hassan, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais kuwa mgombea mwenza huku Chama Cha Mapinduzi kikiweka rekodi ya kuwa na mgombea mwenza mwanamke.
Alisema Samia ameonesha uwezo wa kazi katika nafasi mbalimbali alizopata kuzishika tangu akiwa katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hadi Muungano.
Alifahamisha kwamba Demokrasia ndani ya Chama Cha Mapinduzi imeimarika kwa kiwango kikubwa ambapo nafasi za wanachama mbalimbali kugombea nafasi za juu za uongozi ni kubwa sana ikiwemo wanawake.
Kwa mfano, alisema Chama Cha Mapinduzi kimeweka historia kubwa ya kuteua wanawake wawili kuingia katika hatua ya mwisho ya uteuzi wa tatu bora. ‘’Hicho ndicho Chama Cha Mapinduzi demokrasia yake katika makundi mbalimbali imekuwa kwa kiwango kikubwa ikiwemo wanawake kushirikishwa katika mchakato wa hatua za mwisho na kushika nafasi ya mgombea mwenza,’’ alisema.
Alipoulizwa kuhusu wingi wa wagombea wa nafasi ya juu ya urais, alisema demokrasia katika Chama Cha Mapinduzi imepanuka kwa kiwango kikubwa tofauti na vyama vyengine vya siasa.
Alisema katika mchakato wa nafasi ya urais jumla ya wanachama wa CCM 42 walijitokeza kuwania nafasi hiyo tofauti na miaka ya 2000 ambapo walijitokeza wanachama 17. ‘’Chama Cha Mapinduzi kinajengwa kwa nguvu ya msingi mmoja mkubwa ambao ni demokrasia iliyopevuka inayotoa makundi mbalimbali ya wanachama kuwania nafasi za juu za uongozi,’’alisema.
Akisoma risala ya wananchi wa mikoa sita kichama, naibu katibu mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM Zanzibar), Shaka Hamdu alisema wamefurahishwa na maamuzi ya vikao vya chama kuwateuwa wagombea wa nafasi za juu za urais kwa upande wa Jamhuri ya Muungano na Zanzibar.
Shaka alisema wanachama wa CCM Zanzibar wanaunga mkono uteuzi huo wa majina ya viongozi hao ambao watapeperusha bendera ya chama kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kukileta ushindi chama.
‘’Wanachama wa mikoa sita matumaini yao makubwa kwamba wagombea wa nafasi za urais kuanzia John Magufuli nafasi ya urais wa Muungano pamoja na Dk Ali Mohamed Shein kwa nafasi ya urais wa Zanzibar kwamba ni uteuzi sahihi wa wagombea wenye sifa watakaokiletea chama ushindi,’’alisema.
Mamia ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na wananchi kwa ujumla wamejitokeza katika mapokezi ya mgombea wa urais wa Zanzibar kuanzia uwanja wa ndege wa Abeid Amaan Karume hadi katika makao makuu ya CCM Kisiwandui.

Sentensi 3 kutoka kwa Dr. Wilbroad Slaa kuhusu CCM na ubora wake.
Kwenye mkusanyiko wa stori za mitandao ndani ya siku tano zilizopita
kutoka kwa walichoandika watu mbalimbali maarufu wa Tanzania, zipo pia
hizi tweets za katibu mkuu wa CHADEMA Dr. Wilbroad Slaa.
Ameandika >>> ‘Siku ambayo Watanzania watatambua kwamba walipaswa kuwa mbali sana kimaendeleo, na kujua kwamba kikwazo ni CCM na kukiondoa haiko mbali, hakuna msafi CCM, wala hii si habari mpya… ubora wa CCM ulizikwa na Azimio la Zanzibar 1994, kwa mara nyingine tena tunapaswa kuamua‘
‘Nashukuru UKAWA kwa imani kubwa. Kazi ya mabadiliko iliyoanza 1992 kwa vyama vingi imebakiza miezi michache kushinda. Kura yako ni ukombozi‘ – Dr. Slaa.

Sir Ferguson anawashangaa Juventus kuhusu uamuzi wao kwa Paul Pogba..
Kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United ya Uingereza Sir Alex Ferguson ameshangazwa na uamuzi wa klabu ya Juventus ya Italia kusuasua kufanya maamuzi ya kumuuza kiungo Paul Pogba katika klabu ya FC Barcelona ya Hispania.
Ferguson anaamini ingekuwa busara zaidi kama Klabu ya Juventus ingemuuza kiungo huyo katika klabu ya FC Barcelona ambao wameonesha dhamira ya dhati ya kumuhitaji nyota huyo raia wa kifaransa.
Ferguson anawashangaa Juventus kujishauri kumuuza nyota huyo kwa dau linalokadiriwa kufikia zaidi ya pound milion 50 licha ya yeye kumuacha ajiunge na Juventus kama mchezaji huru mwaka 2012.
Watendaji wa FC Barcelona na watendaji wa Juventus walikutana wiki iliyopita na kukubali kutoa kiasi cha zaidi ya pound milioni 50 kama ada ya uhamisho wa Pogba ambacho Ferguson anaamini walifanya makosa kukataa offer hiyo.
“Ningemuuza Pogba, kama ningekuwa Juve leo hii ningemuacha aende” >>> Ferguson.
Hata hivyo Ferguson aliwapongeza Juventus kwa kutwaa taji la Serie A msimu uliopita na kufika fainali ya klabu bingwa barani Ulaya licha ya kufungwa na FC Ba
“Juve wana
timu bora, wamewahi kutwaa taji la Serie A mara nne mfululizo, kwa
mtazamo wangu walikuwa hawana bahati katika mchezo wa fainali ya klabu
bingwa Ulaya, walifungwa na Barcelona kwa mashambulizi ya kushtukiza
kabla ya hapo waliutawala mchezo” >>> Ferguson.
rcelona.
MAGUFULI NDIYE MGOMBEA URAIS WA CCM 2015
MBUNGE wa Biharamulo Mashariki (CCM) na
Waziri wa Ujenzi, Mhe. John Pombe Magufuli ameshinda katika uchaguzi wa
kumpata mgombea urais wa CCM kwa mwaka 2015. Magufuli ameshinda baada ya
kupata jumla ya kura 2104 sawa na 87.1%, Balozi Amina Salum Ali amepata
kura 253 sawa na 10.5% na Dk. Asha-Rose Migiro 59 sawa na 2.4%.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda ndiye aliyepewa jukumu la kutangaza mshindi aliyepatikana kwa kura za Kikao cha Mkutano Mkuu wa CCM kilichofanyika kuanzia jana na kuendelea leo asubuhi mkoani Dodoma.
KURA ZILIZOPIGWA: 2422
KURA ZILIZOHARIBIKA: 6
KURA HALALI: 2416

Tanzanite yachapwa na Zambia nyumbani
TIMU ya soka ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20, The
Tanzanites, jana ilianza vibaya harakati zake za kusaka tiketi ya
kucheza fainali za Kombe la Dunia baada ya kubugizwa bila huruma mabao
4-0 na Zambia katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Azam Complex
jijini Dar es Salaam.
Ni kipigo kizito kwa sasa Tanzanite inahitaji angalau ushindi wa kuanzia mabao 5-0 wakati timu hizo zitakaporudiana nchini Zambia baadaye.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ni miongoni mwa watu walioshuhudia kipigo hicho cha kusikitisha kutoka kwa wenzao wa Zambia The She-Polopolo.
Tanzanites inayofundishwa na mzalendo, Rogasian Kaijage ilizidiwa karibu kila idara na hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, walikuwa tayari walishapigwa 3-0.
Mabao ya Shepolopolo yaliwekwa kimiani na Memory Phiri dakika ya nne, Irene Lungu katika dakika ya 20 na Barbara Banda dakika ya 33.
Kipindi cha pili, Zambia iliingia uwanjani kwa nguvu na kupata bao la nne huku The Tanzanite wakionekana kuimarika kidogo baada ya kupata maelekezo kutoka kwa benchi la ufundi wakati wa mapumziko.
Wageni Zambia waliandika bao la nne dakika tano tangu kuanza kwa kipindi cha pili lililofungwa kwa penalti na Marry Wilombe. Mwamuzi Refa Batouli Ibrahim wa Sudan alitoa penalti hiyo baada ya Anastazia Anthony kumfanyia madhambi mshambuliaji wa Zambia, Memory Phiri.
Kikosi cha Tanzania; Najjiat Abbas, Zuwena Aziz, Happiness Hezron, Maimuna Hamisi, Anastazia Anthony, Donisia Daniel, Hamisa Athumani, Neema Paulo, Asha Shaaban Hamza/ Janet Cloudy (dk 40), Shelider Boniphace na Stumai Abdallah.
Zambia; Hezel Natasha Nali, Mary Wilombe/Osala Kaelo (dk 75), Margaret Belemu, Martha Tembo, Mlika Limwanya, Lwendo Chisamu, Esther Mukwasa, Irene Lungu, Grace Chanda, Barbara Banda na Memory Phiri/Agnes Musesa (dk 83).

JOSHUA NASSARI APATA AJALI YA CHOPA JIMBONI KWAKE..
Mbunge
wa Jimbo la Arumeri Mashariki, Joshua Nassari amepata ajali ya Helkopta
aliyokuwa akiitumia kufanya ziara jimboni kwake hii leo.
Habari kutoka Arum,eru zinasema kuwa Helkopta hiyo ilipoteza mwelekeo na kwenda kugonga mti na kunasa juu ya mti huo.
Aidha
taarifa hizo zinaeleza kuwa Mbunge huyo kwa Tiketi ya Chadema, na
rubani wake walitoka wakiwa wazima na wapo katika Hospitali ya Kanila la
Kilutheri ya Selian ya jijini Arusha.
Father Kidevu Blog inatoa pole kwa Mbunge huyo na Wapigakura wake wa jimbo la Arumeru Mashariki kufuatia ajali hiyo na tutawaletea taarifa kamili hapo baadae.
Jerry slaa kashea hii ramani ya soko la kisasa la kisutu!
Baada ya kuvunjwa kwa baraza la
halmashauri ya Manispaa ya IIala July 6,2015 na aliyekuwa meya wa
manispaa ya Ilala, Jerry Slaa kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram
amepost miongoni mwa kazi zitakazotekelezwa kwa wananchi ikiwemo huu
ujenzi wa soko la kisutu ambalo muda si mrefu litaanza kufanyiwa
maandalizi ya kujengwa.
‘Soko la
Kisasa la Kisutu Ujenzi wake utaanza muda si mrefu kwa mkopo wa
TIB,litamilikiwa kwa 100% na halmashauri ya manispaa ya Ilala
Nitakumbukwa Kwa Lipi’aliandika @jerrysilaa
Subscribe to:
Posts (Atom)