
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema
kuhusiana na mazungumzo ya nyuklia ya Iran na kundi la 5+1 kwamba,
vikwazo vya kiuchumi, kifedha na kibenki dhidi ya taifa hili vinapaswa
kuondolewa mara moja wakati wa kutiwa saini makubaliano na kwamba,
kuondolewa vikwazo hivyo, hakupaswi kufungamanishwa na utekelezaji wa
ahadi za Tehran. Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amesema hayo
alasiri ya jana wakati alipokutana na viongozi na maafisa wa mfumo wa
Jamhuri ya Kiislamu ambapo alibainisha wazi mistari myekundu ya nyuklia
ya Iran na kusisitiza kwamba, Wamarekani wanataka kuangamiza teknolojia
ya nyuklia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema bayana mbele vya
viongozi na maafisa wa mfumo wa Kiislamu hapa nchini kwamba, Iran
inafuatilia kuhakikisha kwamba, kunapatikana makubaliano mazuri yaani
makubaliano ya kiadilifu, kiinsafu, ya heshima na ambayo yanakwenda
sambamba na maslahi ya taifa hili. Ayatullah Khamenei amesema kuwa,
taifa hili tofauli na wanavyong'ang'ania Wamarekani, halikubaliani na
uwekaji mipaka wa muda mrefu wa miaka 10 hadi 12 na kubainisha kama
ninavyomnukuu: 'kiwango cha miaka ambayo inakubalika tumekwishawaeleza
Wamarekani.' Mwisho wa kunukuu.
No comments:
Post a Comment